Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imepanga kusikiliza maoni ya wadau (Public hearing) kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.8 wa Mwaka 2019 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments)(No.8) Act, 2019, kwa mujibu wa Kanuni ya 84(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.
Mkutano huo wa kusikiliza maoni ya wadau utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 16 Januari, 2020 saa 3.00 asubuhi katika ukumbi Na. 9 Jengo la Utawala Bungeni Jijini Dodoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni yao kabla Muswada huo haujapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau pia yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA.
Baruapepe: [email protected]
Muswada huo pia unaweza kupakuliwa kupitia tovuti ya Bunge, www.parliament.go.tz
Imetolewa na:- Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA.
14 Januari, 2020.