Mwonekano wa sehemu ya msingi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza lililoanza kujengwa Septemba 2019.
Mbunifu Majengo kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Chagu Ng’oma akitoa ufafanuzi kuhusu hatua ulipofikia ujenzi wa jengo hilo.
Sehemu ya mwonekano wa jengo hilo linaloendelea kujengwa.
Baada ya hatua hii ya msingi kukamilika, itafuata hatua ya kunyanyua vyuma ili kupata mwonekano hali wa jengo kama picha inavyoonekana hapo chini.
Mwonekano wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya ujenzi kukamilika. Ujenzi huu utagharimu shilingi bilioni 12, Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela zikichangia Bilioni nne na fedha nyingine ikitolewa na Serikali Kuu. Rais Dkt.John Magufuli aliagiza kujekwa kwa jengo hili wakati akizindua miradi ya afya Julai 15, 2019 katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.