Home Michezo TICTS YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE KUIMARISHA AFYA

TICTS YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE KUIMARISHA AFYA

0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena
bandarini (TICTS), mwishoni mwa wiki walikusanyika kwa pamoja kufanya mazoezi ya
kuimarisha afya zao, mazoezi yanayofanyika kila mwanzo wa mwaka kwa
Wafanyakazi hao kufanya shughuli mbalimbali za michezo ili kuimarisha
afya zao mahala pa kazi.
 

 
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Bonanza hilo, Mkurugenzi wa
Shirika na Maendeleo wa Kampuni hiyo, Donald Talawa amesema
wafanyakazi hao wamekusanyika kwa pamoja kufanya shughuli hizo za
michezo ili kuimarisha afya zao na kuleta tija wawapo kazini.
 

 
“Wafanyakazi wamefanya riadha ya KM 5 na 21, Mpira wa Miguu, kuvuta
kamba na michezo mbalimbali, tunaamini hii italeta tija na ufanisi
mahala pa kazi kwa kufanya hivi mara kwa mara”, amesema Talawa.
 
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wafanyakazi hao, Getrude Lamu amesema wamefanyakazi wamefurahi
sana kufanya mazoezi katika michezo mbalimbali katika bonanza hilo,
amesema wamehamasisha michezo hiyo mahali pa kazi kwa kufanya mazoezi
mara kwa mara.
 

 
“Wafanyakazi wa TICTS katika bonanza la leo wamefika kwa wingi na
wamefurahi sana kufanya bonanza hili, mwezi huu ni mwezi wa mazoezi,
tunashughuru utawala wa Kampuni yetu kuleta kitu hiki kwa Wafanyakazi
wetu”, amesema Getrude Lamu. Endelea kuangalia picha mbalimbali za michezo hiyo hapo chini.