Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawe akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) katika bonanza maalumu la kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Bonanza hilo limehusisha michezo ya aina mbalimbali ikiwemo mchezo wa Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, mchezo wa nage, mchezo wa karata, mchezo wa bao na mchezo wa kuvuta kamba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawe akishuhudia fainali za mchezo wa karata hii leo visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawe akipiga mpira akiwa na timu kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambao wameibuka kidedea dhidi ya timu pinzani kutoka Utumishi.