Balozi Mteule wa Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas
Ndumbaro (Mb) wakati alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akimkaribisha Balozi Mteule wa Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess wakati Balozi Hess katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea na Balozi Mteule wa Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess wakati Balozi Hess alipomtembelea Naibu Waziri katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
*********************************
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria wa Tanzania na Ujerumani ambao ulijengwa tangu enzi za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambapo Tanzania na Ujerumani zina historia ndefu na zimekuwa zikishirikiana kwa miaka mingi katika nyanja za kiutamaduni, kiuchumi na afya.
Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, Mhe. Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa ushirikiano unaolenga kuleta tija katika kuimarisha
uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa haya mawili.