Home Michezo YANGA YAIJIBU SIMBA YALETA WINGA WA TP MAZEMBE

YANGA YAIJIBU SIMBA YALETA WINGA WA TP MAZEMBE

0

Yanga wamewajibu Simba kwa kumleta winga wa TP Mazembe,Owe Bonyanga ametua nchini leo anatarajia kuungana na kikosi hicho visiwani Zanzibar kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Ujio wa winga huyo kutoka TP Mazembe umeijibu Simba ambayo ilimsajili winga Deo Kanda kutoka kwa Mabingwa hao wa DR Congo mwanzoni mwa msimu huu.

Winga huyu ametua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akiwa ameambatana na Meneja wake na kupokelewa na Mkurugenzi wa uwekezaji GSM,Heri Said