*********************************
EMMANUEL MBATILO
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewahikikishia mawakala binafsi wa meli kuwa litafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria iliyopo na halitaingilia shughuli zinazopaswa kufanywa na watu binafsi kama wengine wanavyodhania na kulalamikia uwepo wake.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu wa (TASAC) Mhandisi EMMANUEL NDOMBA amesema kuwa TASAC imeundwa kwa mujibu wa sheria na haijawekwa kwaajili ya kufuta mawakala wengine bali ni kusimamamia shughuli za meli kwa uhakiki na usalama zaidi.
Ameongeza kuwa mpaka kufikia February 17 mwaka huu TASAC itakuwa imeshaanza kushughulikia kazi zote nne walizopewa kwa mujibu wa sheria ambapo watakuwa wanashughulikia meli zote za kijeshi,meli za mafuta, ikiwa ni pamoja na kushughulikia mizigo inayoingizwa na kusafirishwa na jeshi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa udhibiti usafi wa majini DEOGRATIAS MKASSA amesema kuwa hivi sasa wapo mbioni kuweka vigezo vyenye tija kwa watendaji na watoa huduma wote katika shughuli za uwakala wa meli ili kuhakikisha matuzi ya bandari nchini yanaongezeka mara dufu.
Aidha TASAC mpaka sasa wameweza kufuta tozo takribani saba ambazo zimekuwa sumbufu kwa wateja pia imeweza kufanikisha kuwasilisha gawio la faida la takribani billion 10.1 kwa serikali.