Baadhi ya Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zilizowekewa Jiwe la Msingi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi wapili kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Makame Khatib Makame wakati akitembelea Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa na Shirika la Mwezi Mwekundu baada ya kuweka Jiwe la Msingi Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Hussein Ali Mwinyi wakwanza kushoto akikunjuwa kitambaa ikiwa ni ishara ya Kuweka Jiwe la Msingi Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa na Shirika la Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE Khalifa Abdurrahman Almarzooqi akizungumza katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa na Shirika la Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Nyumba za Waathirika wa Maafa ya Upepo Mkali na Mvua za masika zinazofadhiliwa na Shirika la Mwezi Mwekundu Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
……………..
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Hussein Ali Mwinyi amesema kukamilika kwa ujenzi wa nyumba za waathirika wa upepo mkali na mvua za masika kutaweza kutoa fursa kwa wananchi walioathirika na mvua kubwa kuridhia na kufurahia makaazi hayo kwa kaisi kikubwa.
Akiweka jiwe la msingi katika kijiji cha waathirika wa maafa ya mvua huko Nungwi Wilaya ya Kaskazini A amesema hatua hiyo itaweza kuwasaidia wananchi hao kuwa katika makaazi salama na kuweza kuishi kwa amani
Alisema hatua hiyo pia itaweza kuwapunguzia gharama katika kutafuta huduma za kijamii ikiwemo elimu, maji, soko msikiti na huduma nyengine ambazo zitawanufaisha na wananchi wengine tofauti.
Aidha alisema Serikali ya awamu ya saba ilitoa kipaumbele kwa kuanzishwa kamisheni ya maafa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wake juu ya athari zinazowakumba kutokana na maafa hivyo ni vyema wananchi kutojenga sehemu hatarishi mabondeni pamoja na njia kuu za maji ili kuepusha matatizo yatayoweza kuwapata.
“Ni vigumu kuzuiya majanga yasitokee hasa majanga ya kimaumbile kama vile kimbunga, sunami, mafuriko,na mengineyo lakini ni rahisi kuyasuiya maafa yasitokee maafa ambayo yanatokana na binaadamu kwa kujiepusha kujenga sehemu hatarishi. “alisema Waziri wa Ulinzi
Waziri huyo aliishukuru Shirika la Mwezi Mwekundu ya falme za Kiarabu UAE kwa msaada huwo wa kuonyesha hali ya upendo na mshikamano mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi waliyoiyonyesha kuweza kufadhili mradi ambao utaweza kuokoa maisha ya walio wengi.
Hata hivyo Waziri Husein Amewataka wakandarasi kumaliza ujenzi huo kwa wakati uliopangwa ili wahanga wa maafa waweze kufaidika na huduma hiyo kabla ya kufika Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa upande wake Balozi wa Nchi za falme za kiarabu Mhe, Khalifa abdulrahman Almarzouk amesema jumuiya hiyo itaendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kutokana na mahusiano yaliyopo baina ya nchi mbili hizo .
Ameahidi kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya maji, elimu na afya kwa lengo la kuimarisha maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Shaaban Seif Mohamed amesema ujenzi wa kijiji hicho unatokana na athari za upepo mkali na mvua kubwa za masika zilizotokea mwezi April na mei mwaka 2017 ambapo nyumba zipatazo 6,005 ziliathirika kwa Unguja na Pemba.
Alifahamisha kuwa nyumba nyingi zilizoathirika ni zile zilizomo katika maeneo hatarishi yakiwemo mabondeni na njia asilia za maji hali hiyo ilipelekea wana Shirika la Mwezi Mwekundu wa falme za kiarabu kutoa msaada kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema ujenzi wa kijiji hicho umegawika katika awamu mbili tofauti ambapo awamu ya kwanza ni kujenga nyumba I5 za familia thelathini kwa Nungwi Unguja na Tumbe Pemba kwa muda wa mwaka, ujenzi huo unajengwa na Kampuni Samkay Consultant , nyumba ambazo zinavyumba vitatu ukumbi, jiko, choo, na stoo .
Kwa upande wa Wahanga hao waliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mashirika ya Kimaendeleo kwa kuweza kuwaunga mkono katika kipindi ambacho kwao ni kigumu .
Aidha wameomba kuendelea kutoa misaada na mashirikiano kwa jamii katika miradi ya ujenzi wa nyumba hizo ili ziweze kuwasaidia wananchi wanaopata matatizo .
Mmoja na awamu ya pili ni kujenga huduma zilizobaki kwa muda wa miezi kumi ambapo ujenzi huo umegharimu jumla ya shilling bilioni 1,614,299,188 sawa na asilimia sitini.