Joctan Agustino,NJOMBE
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza wakuu wa sekondari zote wilayani kwake kuwapokea wanafunzi ambao hajakamilisha maandalizi ya sare ili wasiweze kuathirika kitaaluma hadi pale wazazi na walezi watakapo zikamilisha.
Msafiri amesema mwanzoni mwa masomo yao wanafunzi wanaotoka familia duni ambazo zipo kwenye maandalizi ya kushona sare hizo waruhusiwe kutumia sare za shule za msingi walizosoma hadi pale watakapo kamilisha ili kuepukana na adha ya kusalia nyumbani na kukosa vipindi
TAARIFA YA JOCTAN MYEFU KUTOKA NJOMBE
Mkuu huyo wa wilaya ya Njombe ametoa agizo hilo wakati akifanya ukaguzi wa miundombinu ya shile za sekondari hususani vyumba vya madarasa, ikiwa wiki moja tu imesalia kwa shule za msingi na sekondari kufunguliwa ambapo amesema utaratibu uliopo umekuwa mwiba kwa familia zenye maisha duni ambazo zimekuwa zikifanya maandalizi kwa kusuasua.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku walimu kuwashinikiza wazazi kuwaandalia ma -COUNTER BOOK watoto na badala yake watumie daftari za kawaida ili kuwapunguzia gharama za elimu wazazi.
Nikas Kapinga ambaye ni kaimu mkuu wa shule ya sekondari Matora na James Tamambele wa sekondari ya Mgala ni baadhi ya shule ambazo zimepangiwa wanafunzi wengi wanaopaswa kuripoti januari 6 kuanza masomo ya kidato cha kwanza wanasema vyumba vya madarasa ni vichache ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi lakini wanafanya kila jitihada kumaliza changamoto hiyo.
Kufuatia upungufu wa vyumba vya madarasa ambao umebainika na kulazimika kuanza ujenzi mara moja kunamfanya afisa elimu halmashauri ya mji wa Njombe Procheus Mguli kumuomba mkurugenzi,wadau na jamii ili kukamilisha na watoto kuanza kutumia pindi shule zitakapofungua.