Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWAKA MPYA

TAARIFA KWA UMMA KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWAKA MPYA

0

 JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA  KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA ULINZI  NA USALAMA LIMEJIPANGA VYEMA KUHAKIKISHA SIKUKUU YA MWAKA MPYA 2020, INASHEHEREKEWA KWA AMANI NA UTULIVU. HIVYO TUWATOE HOFU WANANCHI NA WAGENI WATAKAOTEMBELEA MKOA WETU KWAMBA ULINZI UMEIMARISHWA  WA WAO NA MALI ZAO.

AIDHA, TUTAHAKIKISHA NYUMBA ZOTE ZA IBADA, KUMBI ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE  ULINZI UNAIMARISHWA VYA KUTOSHA KWANI ASKARI WATAKUWA KATIKA DORIA ZA MIGUU, PIKIPIKI, MBWA NA MAGARI KATIKA MAENEO YOTE YA JIJI NA  MKOA WA MWANZA, HIVYO WANANCHI WASIWE NA HOFU YOYOTE  PINDI WATAKAPOKUWA KWENYE IBADA AU BURUDANI MBALIMBALI. PIA TUWATAKE WANANCHI WANAPOKWENDA KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA WASIACHE  NYUMBA ZAO BILA UANGALIZI AU KIZIACHA WAZI KWANI KUNAWEZA KUSHAWISHI WEZI.

 TUWAKUMBUSHE WAZAZI NA WALEZI KUWA PAMOJA NA KUSHEREKEA SIKUKUU HII WASISAHAU MAJUKUMU YAO YA KUWA MAKINI NA WATOTO WAO KWA KUTOWAACHA PEKEE YAO BARABARANI NA KATIKA SEHEMU ZA MICHEZO MFANO MAENEO YA BEACH/MIALO, DISCO TOTO NA KWENYE BEMBEA. PIA NI MARUFUKU KWA MADEREVA  WA VYOMBO VYA MOTO KUENDESHA WAKIWA WAMELEWA AU MWENDO KASI, ENDAPO IKIBAINIKA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO. HATA HIVYO KWA WALE WENYE TABIA YA KUCHOMA MATAIRI BARABARANI WAACHE KWANI NI KOSA KISHERIA.

 UVUMI WA KUTEKWA KWA WANACHAMA WA CHADEMA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAKANUSHA VIKALI  TAARIFA ZILIZOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII NA MAENEO MBALIMBALI KWAMBA WANACHAMA WAWILI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA 

MAENDELEO (CHADEMA)  WAMETEKWA HAPA JIJINI MWANZA.  TAARIFA HIZO SIO ZA KWELI NA LINAOMBA WANANCHI WAZIPUUZE.

TAARIFA KAMILI NI KWAMBA, TAREHE 29.12.2019 MAJIRA YA 15:00HRS HUKO MTAA WA MAHINA, KATA YA MAHINA WILAYA YA NYAMAGANA, KULIPATIKANA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA  KWAMBA KUMEONEKANA WATU WAWILI WALIOHISIWA KUWA SIO WATU WEMA, WAKIWA KARIBU NA HOTEL YA PARADISE NA KUINGIA  NYUMBA ILIYOKUWA JIRANI NA HOTELI HIYO. BAADA YA KUPATIKANA KWA TAARIFA HIZO JESHI LA POLISI LILIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA NA KUFIKA ENEO HILO  NA KUWAKAMATA WATU HAO WAWILI AMBAO KATIKA MAHOJIANO YA AWALI WALIKATAA KUTOA UTAMBULISHO WAO KUWA NI AKINA NANI NA WAMEFIKA MAENEO HAYO KUFANYA SHUGHULI GANI. HIVYO  JESHI LA POLISI LILIWACHUKUA NA KUWAPELEKA KITUO CHA POLISI KATI AMBAPO HATA HIVYO BAADAE WALITOA USHIRIKIANO KWA ASKARI NA KUTAJA MAJINA YAO KUWA WAO NI:- 

  • ABDULKARIM HUSSEIN MURO, MIAKA 31, MCHAGA, AFISA HABARI CHADEMA, KATIBU WA KATIBU MKUU CHADEMA, MUISLAM,  MKAZI WA KINONDONI B –DAR ES SALAAM
  • SAIDI HAIDANI @MALEMBELA, MIAKA 30, MUISLAM, DEREVA WA KATIBU MKUU CHADEMA, MKAZI WA MBEZI, KIMARA – DAR ES SALAAM.

WAMEFIKA MKOANI MWANZA WAKIAMBATANA NA KATIBU MKUU WA CHADEMA MH.JOHN MNYIKA NA BAADA YA POLISI KUJIRIDHISHA KUWA HAWAKUWA WAHALIFU WALIACHIWA HURU KAMA SHERIA ZINAVYOELEKEZA. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KALI KWA  WATU WASIO KUWA NA TAARIFA RASMI NA WENYE TABIA ZA KUZUSHA MAMBO HASA ZA WATU WANAPOKAMATWA WAO KUSEMA KUWA WAMETEKWA NA HIVYO KUZUSHA TAHARUKI KWA JAMII  MATENDO HAYO NI MA KOSA NA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MWANZA KWA UJUMLA SIKUKUU NJEMA YA MWAKA MPYA NA WAISHEHEREKEE KWA AMANI NA UTULIVU.

IMETOLEWA NA;

Muliro J. MULIRO- ACP

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

30 DESEMBA, 2019.