Tuesday, November 10, 2026
Breaking Live updates from Parliament and Government briefings across Tanzania
Full Shangwe Blog
  • Home
  • Beauty
  • Biashara
  • Burudani
  • Entertainment
  • Featured
  • Health
Fullshangwe featured banner Fullshangwe announcement banner
  1. Home
  2. Mchanganyiko

RAIS MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA MALI NA MADENI

By Alex Sonna December 29, 2019 | 4:55 pm





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewasilisha tamko linalohusu Mapato,Rasilimali na Madeni ya viongozi katika Ofisi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria na kikatiba.

Tamko hilo limewasilishwa katika ofisi hizo kanda maalumu ya Dar es salaam na katibu wa Rais,  Bwana Ngusa Samike ambaye ametumwa na Mhe Rais akiwa mapumzikoni Chato na limepokelewa na Kamishna wa Sektretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Jaji mstaafu Harold Nsekela.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea tamko hilo Jaji mstaafu Nsekela amesema kitendo alichokifanya Mhe.Rais kimetekeleza takwa la kikatiba Ibara ya 132 (5) (D) linalowataka viongozi kuwasilisha taarifa za tamko la mapato, Rasilimali na madeni mara kwa mara lakini pia ametekeleza sheria no 13 ya mwaka 1995 kingu cha 9.

Jaji mstaafu Nsekela akatumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wengine kutumia siku 2 zilizobaki kufanya hivyo kabla ya tarehe 31 Desemba katika kutekeleza takwa hilo la kisheria na kikatiba

Related Stories

View all
RAIS DKT. MWINYI: AMANI NA UTULIVU NI MSINGI WA MAENDELEO
Mchanganyiko 1 hour ago

RAIS DKT. MWINYI: AMANI NA UTULIVU NI MSINGI WA MAENDELEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema amani na utulivu ni msingi wa maendeleo ya nchi,…

BENKI YA TADB YAWEKEZA BILIONI 42 KUKUZA KILIMO CHA MATUNDA NA MBOGA MBOGA NCHINI
Mchanganyiko 3 hours ago

BENKI YA TADB YAWEKEZA BILIONI 42 KUKUZA KILIMO CHA MATUNDA NA MBOGA MBOGA NCHINI

Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Alphonce Mokoki, akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha . Happy…

Full Shangwe Blog

Hard-news coverage of Tanzania politics, government, parliament, policy, and public accountability.

[email protected] +255 700 000 000

News

  • Politics
  • Government
  • Parliament
  • Policy

Topics

  • Elections
  • Budget
  • Regions
  • Diplomacy

Readers

  • About Us
  • Advertise
  • Contact
  • Submit News

Follow

© 2026 Full Shangwe Blog. All rights reserved. Design by Webline Africa Limited
Privacy Policy Terms Editorial Policy