Mbunge wa jimbo la Busega,Mkoani.Simiyu Mhe. Dkt. Raphael Chegeni.
*************************************
MBUNGE wa jimbo la Busega, lililopo mkoa wa Simiyu, Mhe. Dkt. Rafael Chegeni anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha kuhitimisha tamasha kubwa la kukuza na kuendeleza Utalii la ‘LAMADI UTALII FESTIVAL.’
Mwenyekiti wa Kamati wa Tamasha hilo, Mkuu wa Wilaya ya Busega Bi. Tano Mwera akizungumza katika mahojiano maalum na radio Bunda (Bunda FM), ameeleza kuwa, wanamtarajia kuwa na Mbunge wa jimbo hilo katika viwanja vya shule ya Itongo siku ya Januari Mosi, 2020.
“Siku ya kilele Januari Mosi tutajumuika pamoja na mgeni rasmi ambaye atalifunga tamasha letu, Mbunge Dkt. Rafael Chegeni katika viwanja vya Shule ya Itongo.” Alieleza Mkuu wa Wilaya, Bi. Tano Mwera.
I
Katika siku hiyo ya kilele pia litakuwa na shughuli za safari za kitalii ikiwemo ya kwenda Hifadhi ya Serengiti kwa malipo ya gharama nafuu.
“Siku ya kilele Januari Mosi, 2020 tutakuwa na tukio la kwenda hifadhi ya Serengeti na gharama ni Tsh. 55000, kwa kila Mtanzania lakini watoto 10 wa mwanzo wao watalipiwa Tsh. 50,000 pekee kama ofa. Gharama hiyo itajumlisha usafiri wa kutoka na kurudi Lamadi, ada ya kiingilio, chakula cha mchana, vinywaji laini.
Tunatoa wito watu kujitokeza kulipia mapema kwani idadi ni nafasi ya watu 30. safari ya siku moja kutoka saa 12 alfajili na kurudi Saa 12 jioni.” Alieleza Mkuu wa Wilaya, Bi. Tano Mwera.
Awali kabla ya kilele, tamasha hilo, Desemba 31kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo: Utalii wa kuzunguka ziwa Victoria na boti ‘Boat Cruising’ ambapo gharama itakuwa Tsh. 10,000 kwa Mtanzania na muda ni masaa matatu kwenye maji.
Pia kutakuwa na Biking kwa gharama ya Tsh. 5000 kwa kila Mtanzania ikijumuisha kukodi baiskel kwa nusu siku pamoja na maji ya kunywa ambapo itaanza saa 12 asubuhi hadi mida ya saa 5 asubuhi.
Mbali na shughuli hizo za Utalii, Wananchi watapata kuona shughuli mbalimbali ikiwemo burudani, michezo pamoja na kufanya manunuzi ya bidhaa.
“Unakosaje Lamadi Utalii Festival.!! Vyakula vya asili, Nyama choma,Uchomaji wa samaki (Sato Corner).
Wasanii wa kila aina. Wachoraji, wasusi, wachonga vinyago na mengine mengi.” Alieleza DC Tano Mwera.
Aidha, katika tamasha siku ya mkesha wa Mwaka Mpya kutakuwa na usiku maalum wa ‘Karaoke Night’ ambao watu mbalimbali watapata wasaha wa kuimba nyimbo mbalimbali na kufurahia pamoja mwaka mpya.
Tamasha hilo mwaka huu ni la kwanza na kudhaminiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wadau wengine mbalimbali huku likiwa na Kauli mbiu ya “Utalii wa Ndani Unawezekana”.