Home Michezo TASWA KUFANYA MKUTANO MKUU JANUARI 12,2020

TASWA KUFANYA MKUTANO MKUU JANUARI 12,2020

0

MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), uliokuwa ufanyike Jumapili wiki hii sasa utafanyika Januari 12, mwakani.

Hatua ya kusogeza mbele mkutano inatokana na maombi ya baadhi ya wanachama, ambao walichelewa kuthibitisha ushiriki wao kwa muda uliokuwa umepangw awali, hivyo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwapa nafasi.

Lengo la mkutano huo  ni kujadili masuala mbalimbali ya chama, ambapo pia utapokea taarifa kutoka Kamati ya Marekebisho ya Katiba iliyoundwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na pia utapokea mapendekezo kutoka Kamati ya Utendaji ya TASWA  inayomaliza muda wake.

Watakaohudhuria Mkutano Mkuu Maalum ni wanachama wote walio katika leja baada ya kushiriki uchaguzi wowote wa TASWA kuanzia mwaka 2004, 2007, 2010, 2014 na wanachama wapya wote walioingia kuanzia mwaka 2015 hadi Juni mwaka huu.

Kwa mazingira hayo ili mkutano ufanyike kwa ufanisi ni vyema yeyote mwenye nia ya kushiriki athibitishe kwa maandishi akitaja jina lake na chombo na kutuma kwa email: [email protected] au [email protected] au [email protected],   ili taratibu nyingine ziendele. Mwisho wa kuthibitisha ushiriki sasa ni Desemba 31 mwaka huu.