Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqaro akianza ukaguzi wa mabanda ya wajasiliamali wanawake kabla ya kufunga Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqaro akiangalia bidhaa aina ya mvinyo unaotengenezwa na Bi. Magreth Ibrahim wa Joma Enterprises kabla ya kufunga Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqaro akianza ukaguzi wa mabanda ya wajasiliamali wanawake kabla ya kufunga Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqaro akitoa ushauri kwa wajasiliamali wanawake wanaotengeneza Nguo aina ya batiki wakati wa ukaguzi wa mabanda ya wajasiliamali wanawake walioshiriki Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini Arusha.
………………
Na Mwandishi wetu Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqaro amewataka wanawake wajasiliamali Mkoani Arusha kuwa wazalendo kwa kulipa kodi pale biashara yao inapokuwa kubwa kwa kuwa jukumu la kujenga Nchi ni la kwetu sote akionya kuwa baadhi ya watu wasidhani hawana jukumu la kujenga Nchi.
Pamoja na mambo mengine Bw. Daqaro amewataka wanawake wajasiliamali hao kutumia fursa waliyopata ya elimu ya ujasiliamali kuwasaidia kuwekeza ili waweze kubadilisha maisha yao, familia na Taifa kwa ujumla.
Bw. Daqaro Ameyasema hayo wakati wa hotuba yake yakufunga Kongamano la Siku mbili la uwezeshaji wanawake kiuchumi waliokusanyika kutoka Wilaya za Mkoa wa Arusha na kuongezewa ujuzi kwa kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali.
Aidha Bw. Daqaro amewataka Wajasiliamali hao kurasimisha biashara ili waweze kuwa katika mfumo unaojulikana unaotambulika na serikali ili wote tushirikiane kujenga Taifa letu na kuwataka kutambua kuwa inabidi kushirikiana na serikali kujenga Nchi hii.
Bw. Daqaro amewataka wajiasiliamali hao wanawake kuzingatia viwango vya ubora katika bidhaa zao ili ziweze kushindana katika soko kwa kuhakikisha wanakuwa na vifungashio imara na bora ili bidhaa zao ziweze kukidhi ubora na kushindana katika soko.
Amelitaka Shirika la Viwanda vidogo Nchini SIDO kuendelea kutoa elimu ya biashara kwa vikundi vya akina mama ili viweze kuzalisha bidhaa bora zinazoweza kushindana katika Soko.
Akiongea wakati wa kufunga Kongamano hilo Bi. Mboni Mgaza Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii amesema washiriki wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake kiuchumi walifikia 200 na wamepatiwa mafunzo mbalimbali ua ujasiliamali pamoja na uzalishaji bidhaa kwa lengo la kukuza uwezo wao wa kiuchumi.
Bi. Mboni Mgaza pia wanawake kupitia Kongamano hilo wameweza kuonesha na kuuza bidhaa zao lakini pia kuna baadhi ya wanawake ambao wamepatiwa mafunzo na Taasisi mbalimbali ambazo zilitoa jumla ya mada 13.
Naye Mshiriki wa Kongamano hilo Bi. Irene Paranjo amesema Kongamano hilo limeleta faida kwa wanawake hao kwani wameweza kujenga mtandao lakini pia kubadilishana Mawazo ya namna ya kuboresha biashara zao lakini pia imekuwa ni fursa kwao kukutana na viongozi wa juu ambao wamehaidi kuwasaidia katika juhudi za Serikali za kuwezesha wanawake kiuchumi.
Serikali imekuwa ikitoa Mikopo kupitia Serikali za Mitaa kwa Wanawake waliokatika vikundi vya hisa na ujasiliamali kwa lengo kuwezesha wanawake kiuchumi na tayari Serikali tayari kupitia mapato ya Halmashauri zote Ncini inatenga asilimia kumi ya mapato yake kwa lengo la kuwezesha wanawake vijana na walemavu.