Mwezeshaji wa mafunzo ya Elimu Dkt. Alfred Hugo kutoka chuo kikuu cha Dodoma akitoa ufafanuzi kuhusiana na mafunzo ya ualimu katika chuo cha Ualimu Bustani kilichopo wilayani chemba.
Mwalimu wa shule ya msingi Bangumo Bi. Nuru Mwandelile akieleza namna alivyonufaika na mafunzo katika chuo cha Ualimu Bustani kilichopo wilayani chemba.
Mwalimu wa somo la hisabati Bw. Anold Waziri akitoa ufafanuzi wa zana na ujuzi alioupata kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika chuo cha Ualimu Bustani kilichopo wilayani chemba.
Baadhi ya walimu wakiwa kwenye chumba cha darasa wakiendelea na mafunzo kama ilivyo ada
……………….
Na.Boniphance Richard,Chemba
Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na serikali ya Canada nchini, imeandaa mafunzo kwa walimu somo la hisabati wa shule za sekondari na msingi zenye ufaulu hafifu kwenye mitihani ya kumaliza Elimu ya msingi na kidato cha nne.
Akizungumza mapema jana, mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka chuo kikuu cha Dodoma Dkt. Alfred Hugo alisema mafunzo hayo yanaendeshwa kwenye halmashauri 20 zenye wanufaik a zaidi ya 800 ambapo kuna halmashauri 8 za shule ya msingi pamoja na halmashauri 12 za sekondari zenye ufaulu hafifu wa mitihani ya taifa.
“ Wizara kupitia wameona ni vyema kutoa mafunzo katika wilaya ya chemba kwa maana ya walimu wa shule ya msingi na sekondari ambapo ni jumla ya walimu 62 wa shule za msingi na sekondari walimu 38” alisema Hugo
Aidha aliongeza kuwa mradi wa wawezeshaji na uendeshaji wa elimu katika shule za sekondari na msingi, umeongezeka kwenye wilaya ya chemba baada ya mradi kupanua wigo kutokana na uhitaji mkubwa wa walimu zaidi ambapo ni imani yao kama wawezeshaji wa mafunzo hayo kwamba walimu wataweza kufundisha vyema na kutekeleza yale yote waliowaelekeza.
Pia mwezeshaji kutoka chuo kikuu cha Dodoma, alisema mafunzo hayo yameambatana na mitaala maalumu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ambayo itasaidia walimu kufundisha kwa njia ya vitendo zaidi tofauti na awali ambapo walimu walikua wanatumia njia ya kanuni kutatua masuala ya hisabati.
“Mitaala yote miwili tiliyoandaa inamjengea mwalimu uwezo wa kuweza kujenga dhana halisi ya kile kitu ambacho anaenda kukifundisha kwa maana ya kupanua wigo wa uelewa kwa kutumia zana ambazo zipo karibu na mazingira yao haswaa mazingira ya vijijini” aliongea Dkt
Kwa upannde wake mwalimu wa shule ya msingi Bangumo wilayani chemba, madam Nuru Mwandelile alisema kupitia mafunzo hayo amepata mbinu mbalimbali pamoja na zana nyingi za ufundishaji wa somo la hisabati ambalo linaonekana kuwa na mtazamo hasi wakati wa ufundishaji.
“Katika baadhi ya mada ni ngumu sana mfano kufundisha hesabu za hasi na chanya lakini kumbe kuna zana ambazo zinatuzunguka katika mazingira yetu za kumfundisha mwanafunzi na akaelewa vizuri “ alisema Nuru
Sanjari na hayo, mwalimu Anold Waziri kutoka shule ya sekondari alieleza kuwa somo la hisabati limepata fursa kubwa kutoka kwenye mradi wa mafunzo hayo ambapo wameongeza ujuzi wa kufundisha kwa njia ya vitendo ambapo baadhi ya zana kama vile namna ya kutafuta ujazo, eneo, mzingo na maumbo kwa kutumia mazingira husika yanayowazunguka wanafunzi kwa kupata maarifa na ujuzi wa kuliele wa somo la hesabu.“Hisabati ni maisha” alisema Anold