Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha ,Richard Kwitega akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi hicho kilichofanyika mkoani Arusha leo.(Happy Lazaro).
Wadau mbalimbali wakiwa katika ufunguzi wa Kikao kazi kwa wadau na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali ya Kanda ya Kaskazini kilichofanyika Mkoani Arusha kwa lengo la kutoa maoni ya mapitio ya Sera ya Jinsia na wanawake.(Happy Lazaro)
**********************************
Happy Lazaro,Arusha.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na watoto imeamua kufanya Tathimini ya Sera ya wanawake ya mwaka 2000 ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia kwa karne ya 21 ili kuwezesha kukua Kiuchumi.
Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi kwa wadau na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali ya Kanda ya Kaskazini kilichofanyika Mkoani Arusha kwa lengo la kutoa maoni ya mapitio ya Sera ya Jinsia na wanawake ,Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameeleza Ushiriki wa Jamii katika kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kutafuta ufumbuzi itapanua wigo katika kudurusu na kupata Takwimu sahihi kuendana na ukuaji wa utandawazi na kuwa na mikakati ya kuiwezesha Nchi kufikia malengo waliyojiwekea.
Ameeleza kuwa, Kanda ya kaskazini inakadiriwa kuwa na watu Takribani Milioni 9 kwa mwaka 2019 ambapo Tathimini hiyo kwa sasa itasaidia kujua ongezeko kwa wanawake kwani Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 kupitia mpango wa pili wa Maendeleo ya miaka 5 itawezesha kuangalia muafaka wa mabadiliko ya ndani ya nchi ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi, Sera ya kilimo kazi ,mabadiliko ya siasa hususani kwa kipindi hiki nchi inapoelekea katika Sera ya Uchumi wa kati wa Viwanda ikiwa ni Dhamira ya serikali ya Awamu ya 5.
Mkurugenzi msaidizi idara ya maendeleo ya jinsia,wizara ya afya maendeleo ya jamii ,jinsia ,wazee na watoto, Grace Mwangwa amesema ni miaka 19 sasa tangu sheria hiyo kuwepo ,na wanahitaji kuifanyia Maboresho sera inayomwangalia mwanamke na Mwanaume ikiwemo makundi maalumu pamoja na vijana.
Ameongeza kuwa , tayari wamekwishazifikia Kanda 4 ikiwemo Kanda ya Kati,Kanda ya ziwa,Kanda ya mashariki na sasa ni Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha ,Kilimanjaro Tanga na Manyara.
Nay pple mmoja wa Washiriki wa Semina hiyo Siparo Lejula kutoka wilaya ya kiteto Mkoani Manyara amesema kuwa, kipindi cha nyuma Jamii ya kifugaji ilikuwa haipewi kipaumbele na kubaguliwa hata katika Upande wa umiliki wa Ardhi ,Chakula na kuchangamana na wanaume jambo ambalo kwa sasa hali hiyo imekomeshwa na kupewa kipaumbele kikubwa huku akiishukuru serikali kufanya mapitio hayo ya Sera .
Naye Profesa Lindah Mhando Mtaalamu mwelekezi wa mapitio ya Sera ya wanawake Taifa ,amesema yapo maeneo mengi yamejitokeza katika kila sekta na taaluma katika kuleta usawa wa kijinsia,hivyo Maeneo hayo Takribani 24 yatapewa kipaumbele katika Sera hiyo ikiwemo Sera ya jinsia Maendeleo mijini na vijijini, haki za binadamu,Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya Nchi Pamoja na kumwangalia mtoto wa kike na wa kiume na hii ni ili kuwa na Tanzania mpya na uchumi endelevu.