Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo, ameagiza kufanyika uchunguzi wa fedha zote za miradi ya maendeleo wilayani Nanyumbu kufuatia taarifa za ufujaji wa fedha za miradi zilizo elekezwa wilayani humo.
Waziri Jafo amsema kuwa timu hiyo itatoka TAMISEMI Makao makuu itaanza kazi mara moja ili kujiridhisha juu ya tuhuma hizo na endapo itabainika kuwa zina ukweli hatua mbalimbali zitachukuliwa .
Jafo ametoa maagizo hayo leo wilayani humo wakati wa ziara ya kikazi mkoani Mtwara.
Aidha Waziri Jafo amefanya ziara wilayani Masasi na kufanya ukaguzi wa ujenzi wa shule ya mfano ya Kisasa ujenzi wa kituo cha Afya Chihungutwa, pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya masasi.
Katika ukaguzi huo Jafo amechukizwa na wizi wa vifaa vya ujenzi uliofanywa na wananchi katika kituo cha Afya Chihungutwa na ameagiza wananchi hao kukamilisha ujenzi huo kwa fedha zao wenyewe kwani serikali ilishapeleka shilingi milion 400 hivyo haita endekeza tabia za baadhi ya watu wanaoleta masihara katika maendeleo.
Aidha, Jafo amempongeza mbunge wa Lulindi Mhe. Dismas Bwanausi kwa kujituma kwake katika kuwapambani wananchi wake katika maendeleo.