Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Ntela Mwampamba (kulia) akitoa utambulisho wa meza kuu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Afisa mradi wa na Elimu ya Afya na Ukimwi kutoka UNESCO, Jennifer Kotta (kushoto) akitoa utambulisho kwa mgeni rasmi na timu nzima kutoka Unesco wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe. Kulia ni mshehereshaji wa uzinduzi huo kutoka UNESCO, Bi. Rose Mwalongo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) Mwita Mwaitara akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Mh. Suleiman Jafo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe. Kulia ni mshehereshaji wa uzinduzi huo kutoka UNESCO, Bi. Rose Mwalongo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Mathias Herman akitoa salamu za UNESCO wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afya,
Ustawi wa Jamii Jinsia, Wanawake, Vijana na Watoto (BAKWATA), Bi. Asina Shenduli akisoma tamko la viongozi wa dini wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii), Bi. Anna Mhina akitoa taarifa za kitaifa na jitihada zinazofanyika kupunguza ukubwa wa tatizo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kisarawe, Ibrahim Msafiri akitoa taarifa ya kiwilaya (Kisarawe) na jitihada zinazofanyika kupunguza ukubwa wa tatizo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Binti Recho Mdea akitoa ushuhuda wa maisha yake na changamoto alizopitia kama binti na kuhamasisha wengine kuwa jasiri kama yeye wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Baadhi ya wadau kutoka sekta mbalimbali nchini walioshiriki uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi Kisarawe wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali zinazohamasisha kutokomeza na kukomesha mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mwita Mwaitara akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO huku Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kulia) pamoja na Diwani wa kata ya Kisarawe Abel Mudo (kushoto wa kwanza) wakishuhudia tukio hilo katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, Kisarawe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mwita Mwaitara akifunua pazia kwenye ubao maalum wa kuweka saini kama ishara ya kuzindua kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO huku akisaidiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kulia) Mwakilishi wa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Mathias Herman (wa tatu kushoto) katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mwita Mwaitara akiweka saini kwenye bango maalum linalosema “Nina ahidi kusaidia juhudi za kupambana dhidi ya mimba za utotoni “, kama ishara ya kuzindua kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akiweka saini kwenye bango maalum linalosema “Nina ahidi kusaidia juhudi za kupambana dhidi ya mimba za utotoni “, kama ishara ya kuzindua kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mwakilishi wa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Mathias Herman akiweka saini kwenye bango maalum linalosema “Nina ahidi kusaidia juhudi za kupambana dhidi ya mimba za utotoni “, kama ishara ya kuzindua kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni kwa ufadhili wa UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na sehemu ya wadau wa sekta ya elimu na afya pamoja na wanafunzi wa shule za msingi waliohudhuria uzinduzi kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walioshiriki uzinduzi kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Unesco walioshiriki uzinduzi kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi wakitoa burudani ya wimbo maalum wa kupinga mimba za utotoni wakati wa uzinduzi kampeni ya taifa dhidi ya mimba za utotoni iliyofadhiliwa na UNESCO kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chanzige, wilayani Kisarawe.
Mwita ataka halmashauri kuweka bajeti kulinda wasichana
Na Mwandishi wetu, Kisarawe
Halmashauri nchini zimetakiwa kurahisisha uratibu na usimamizi wa shughuli za ustawi wa jamii kwa kuimarisha idara yake na kuwezesha bajeti ili changamoto za mimba za utotoni ziweze kushughulikiwa kikamilifu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) Mwita Mwaitara wakati akizindua kampeni dhidi ya mimba za utotoni kulikofanyika wilayani Kisarawe.
Kampeni hiyo inaendeshwa na Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kisarawe,kwa kusaidiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kamati ya ushirikiano ya dini mbalimbali.
Uzinduzi huo uliambatana na kongamano lililolenga kuchambua na kuona njia bora za kukabiliana na mimba za utotoni wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani na Tanzania kwa ujumla wake.
Kampeni hiyo iliyobeba kauli mbiu ya “Hebu Tuzungumze” kwa lengo la kuvunja ukimya inasema kwamba hali si nzuri kwa kuwa kwa taarifa ya BEST ya mwaka 2018 inaonesha kwamba wasichana 4,800 wameshindwa kuendelea na shule kutokana na ujauzito.
Ofisa Programu mawasiliano wa UNESCO Rose Mwalongo alisema kwamba mimba hizo si za hiari bali zinatokana na ukosefu wa elimu na hata umaskini. Pia imeelezwa kuwa nchini Tanzania asilimia 12 ya wasichana kati ya miaka 15-24 huanza kufanya mapenzi kabla hawajatimiza miaka 15.
Katika kongamano hilo ilielezwa kuwa mimba za utotoni zimekuwa mwiba katika maendeleo ya mtoto wa kike na taifa kwa ujumla hivyo ipo haja ya kukabiliana nazo kwa kuwa na bajeti kamili ya ustawi.
Mwita amesema kwamba wakati serikali kuu inafanya kila linalowezekana kuweka mazingira sawa ya kumwendeleza mtoto wa kike ni wa jibu wa jamii kuhakikisha kwamba mtoto huyo analindwa na taratibu zilizopo za ulinzi wake zinafuatwa.
Alisema serikali imeridhia Azimio la Umoja wa Mataifa la ulinzi wa mtoto la mwaka 1989 na kwamba sheria zilizopo zimelenga kuhakikisha kwamba mtoto analindwa dhidi ya maslahi yake ya baadae kama mimba , ndoa za utotoni na utumikishwaji.
Alisema juhudi lazima zifanyike kuondoa changamoto zinazosababisha mimba za utotoni ambapo kwa wilaya ya Kisarawe kwa mwaka huu pekee kumekuwepo na mimba 40 ambapo shule za sekondari wamepatikana 38 na shule za msingi 2.
Alisema kama taifa, inatakiwa kuhakikisha kwamba changamoto ya ndoa za utotoni zinaondolewa na mabinti wanapata nafasi ya kujipangia maisha yao.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alikiri kukithiri kwa vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo mimba za utotoni, na ubakaji .
Alisema jumla ya wanafunzi 40 kutoka shule za sekondari na wawili shule za msingi walikatisha masomo baada ya kupata ujauzito.
Alibainisha kuwa kati ya matukio hayo 40, ni matukio nane tu yaliopelekwa mahakamani na kutolewa hukumu .
Alifafanua kuwa kesi nyingi zinashindwa kuendelea kwasababu ya wanafamilia kulindana hivyo hutoa vitisho kwa mtoa ushahidi na kumfanya kushindwa kusimamia ukweli.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya mimba za utotoni katika wilaya hiyo, wilaya imeanzisha kampeni maalumu ijulikanayo “ukatili wa kijinsia Kisarawe sasa basi”.
“Hatutavumilia yeyote vatakayehusika kwa nanma yoyote kusababisha mimba kwa wananfunzi, na kushindwa kufikisha kesi sehemu husika” alisema.
Jokate alisema wilaya imeamua kuingilia kati kwa sababu wamebaini wazazi na wanafamilia wamekuwa wakikwamisha kesi hizo kwa lengo la kulindana.
Kwa mujibu wa mada iliyowasilishwa na Anna Mhina, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) asilimia 37 ya wasichana waliolewa kabla ya kufikisha miaka 18 na mikoa yenye takwimu za juu ilikuwa Shinyanga (59%), Tabora (58%), Mara (55%), Dodoma (51%) and Lindi(48%).
Aidha takwimu za mwaka 2010 zimeonyesha kuwa asilimia 27 ya wanawake wenye umri wa miaka kati ya 15 na 19 walipata mimba na kuzaa kabla ya kufikisha miaka 18. Mikoa yenye kiwango cha juu cha mimba za utotoni ni Katavi (45%), Tabora (43%), Morogoro (39%), Dodoma (39%) na Mara (37%) (TDHS 2015/16).
Mhina alisema umaskini, ukimya miongoni mwa wanajamii katika kutoa taarifa za matukio ya ukatili punde yanapotokea, mmomonyoko wa mfumo wa malezi kwenye jamii unaofanya watoto wengi kukosa ulinzi na hivyo kujikuta wakijitumbukiza katika mazingira ya uharibifu.
Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na watu zaidi ya 200 kutoka Pwani, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Tamisemi, viongozi wa kidini, viongozi wa jamii, walimu, wazazi, vyombo vya habari wanafunzi na vijana kutoka Kisrawe na nje ya Kisarawe.
Katika kongamano hilo watu wa dini walitoa azimio la kuunga mkono mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni na kwamba watahimiza waumini wao kuhakikisha wanasaidia ulinzi kwa mabinti.
Kauli hiyo iliwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afya, ustawi wa jamii, jinsia, wanawake, vijana na watoto Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Asina Shenduli.
Alihimiza wananchi kutambua kuwa hilo ni tatizo na kutaka elimu iendelee kutolewa kuhusu namna ya kumlinda mtoto wa kike.
Katika kongamano hilo kumetajwa maeneo manane ya kuimarisha ikiwamo uchumi kwa kuongeza kipato cha familia na kuondoa mila na desturi zenye madhara.
Eneo jignine ni kutengeneza mazingira salama kwa kufanya mapitio ya sheria ndogondogo na kanuni zinazohusu matumizi ya maeneo ya umma na maeneo ya burudani kuwa salama kwa watu wote, ukaguzi wa maeneo ya kazi na kuboresha stadi za maisha shuleni