Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kuangalia chanzo cha maji cha Milima ya Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo mitambo itajengwa kwa ajili ya kusambaza maji katika mkoa wa Morogoro.
Mhandisi wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana na umuhimu chanzo cha maji cha uhakika kwa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Juma Oweso ya kwenda kuangalia chanzo hicho cha maji.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akipumuzika na viongozi mbalimbali wakati kupanda mlima wa kufikia chanzo cha maji katika eneo Hululu.
Sehemu ya chanzo ambapo mtambo utajengwa kwa ajili ya maji katika mkoa wa Morogoro.
******************************
MKOA wa Morogoro hivi karibuni itaondokana na tatizo la maji kutokana na kupata chanzo cha uhakika kutoka milima ya Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo bwawa la Mindu litatumika kama ziada ya Maji.
Chanzo cha maji hicho kimefikiwa na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso wakati alipokwenda kuangalia chanzo hizo na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa).
Katika ziara ya Naibu Waziri Aweso aliwaagiza na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa) kuandika andiko kwa kina ili kuwekeza miundombinu katika chanzo cha maji cha milima Ulugulu katika eneo la Hululu.
Viongozi wa eneo la chanzo cha maji walieleza kuwa Naibu wa Waziri huyo ni kiongozi wa kwanza kufika eneo la chanzo cha maji tangu dunia iiumbwe na kudai kuwa serikali ya awamu ya Tano ina udhubutu wa viongozi katika utendaji wa kuhakikisa wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanaondokana na tatizo la maji.
Naibu Waziri Aweso amesema kuwa kutokana na chanzo cha maji hayo kuwepo kwa muda wote kulikuwa hakuna sababu ya kutumia Bwawa kwani mabwawa huwekwa sehemu ambayo ni kame hivyo mkoa wa Morogoro si Kame kwa kuwa na chanzo cha maji kinachotegemea bwawa.
Amesema kuwa chanzo hicho cha maji katika milima ya Ulugulu ni kufikisha Morogoro ni jirani ukilinganisha na mradi wa maji wa Ziwa Victoria kutolewa mwanza na kwenda katika mikoa mbalimbali ambayo ilikuwa na ukame wa maji na hawakujua watapata katika chanzo kipi.
Nae Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani alimweleza kuwa chanzo hicho kinatokana na utunzwaji wa mazingira na kutaka wananchi waendelee kulinda vyanzo vya maji.
Ngonyani amesema kuwa kuna miradi mbalimbali ya miundombinu katika Mkoa wa Morogoro lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kwenda kwa kasi katika ujenzi wa viwanda ambavyo kuendelea kwake kunatokana na upatikanaji wa maji.
Mhandisi Ngonyani amesema kuwa wanapokea maagizo ya Naibu Waziri Juma Oweso na kuahidi watafanyia kazi kwa kuandika andiko la mradi kwa kushirikiana na Moruwasa ikiwa chanzo hicho kuanza kufanyiwa kazi.
“Ninaamini chanzo hiki kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro na kuwa historia kutegemea bwawa kwa mkoa wenye vyanzo vya maji Lukuki hivyo bonde litaendelea kuhakikisga vyanzo vya maji vinalindwa vizazi kwa vizazi”amesma Ngonyani.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwalimu Mohamed Utaly amesema kuwa chanzo cha maji hicho kwa Mkoa wa Morogoro kwa serikali ya awamu chanzo cha maji kitajengwa.