Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Magomeni ambapo wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya wakikagua mradi huo.
Muonekano wa Kituo cha Afya cha Kigogo ambapo wa jumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Kinondoni walifanya ziara hap jana.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Harlod Maruma, akiwa na Mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia mwnye tisheti ya njano, akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipokuwa katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Makumbusho.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Harlod Maruma, mwenye miwani akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipokuwa wakikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Makumbusho. Mweyeshati jeupe ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akiangalia mtambo wa kuchakata kokoto katika ujenzi wa kituo cha Afya cha Makumbusho, walipokuwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni, Sure Mwasanguti wa kwanza kulia akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo ,wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya Halmashauri hiyo, katikati mwenyemiwani ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya , Said subety .
*****************************************
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni jana imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi sita iliyopo katika Kata tano kati ya kata 20 zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Ziara hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Harlod Maruma, ilihusisha viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, Mstahiki Meya Benjamini Sita, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk. Patricia Henjewele, Mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia, watendaji pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali.
Aidha kamati hiyo ilitembelea mradi wa Kituo Cha Afya Cha Kigogo kinachojengwa kwa shingili milioni 700 ambapo kati ya fedha hizo shilingi milioni 400 ni pesa kutoka Serikali kuu, shilingi milioni 300 ni pesa zinazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Kamati hiyo ilitembelea mradi mkubwa wa Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi Bilioni 8.9 ambapo kamati hiyo ilieleza kuwa imeridhishwa na hatua ya soko hilo ilipofikia kwa sasa na hivyo kutumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi Ndugu. Aron Kagurumjuli na watendaji wake.
Kamati hiyo pia ilitembelea mradi wa ujenzi wa vyumba sita vya madarasa ya ghorofa shule ya Sekondari Mzimuni, ambapo Mkuu wa shule hiyo , Yahaya Kirondo alisema kuwa kulingana na kasi ya ujenzi unavyo endelea hadi kufikia Januari 2020 wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo wataanza kutumia madarasa hayo.
Aidha kamati hiyo pia ilitembelea ujenzi wa Zahanati ya Magomeni, Makumbusho ambapo kwa mujibu wa mkandarasi mshauri anayesimamia ujenzi wa Zahanati hizo, alisema kuwa hadi kufikia Aprili 2020 zitakuwa zimekamilika na hivyo wananchi kuanza kupata huduma.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Daniel Chongolo aliieleza kamati hiyo kuwa, kumalizika kwa Zahanati hizo kutasaidia kuwa rahisishia wananchi kupata huduma za karibu katika Zahanati hizo badala ya kwenda moja kwa moja katika Kituo Cha Afya cha Magomeni au Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala.
Mhe. Chongolo alisema kuwa, Zahanati hizo pia zitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Magomeni na maeneo mengine kwa kuwa eneo hilo linawakazi wengi na kwamba ha kukuwa na Zahanati zaidi ya Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Kituo cha Afya Cha Magomeni.
Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi wa barabara zinazo simamiwa na DMDP ambazo ni Shekilango yenye urefu wa kilomita 3.7, Barabara ya Akachube yenye urefu wa kilomita 0.94, barabaa ya TRA yenye urefu wa kilomia 1.1, barabara ya Sinza Mori yenye urefu wa kilomita 0.93 na Igesa yenye urefu wa kilomita 0.64.
Imetolewa leo Disemba 19
Na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni.