Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene akiwa katika skuli ya maandalizi ya Kangagani wakati wilayani
Wete, Pemba wa ziara ya kutembelea miradi ya Mfuko wa Jimbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene akifurahia jambo na wabunge alioambatana nao kwenye ziara ya
kukagua miradi ya Mfuko wa Jimbo wilaya za Wete na Chakechake mara baada
ya kuwasili Ofisi za Makamu wa Pili wa Rais Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara wilayani
Chakechake. Kulia kwake ni Mbunge wa Mtambile, Mhe. Masoud Abdallah
Salim.
Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Lupi Mwaikambo akifafanua jambo katika kikao cha majumjuisho ya ziara ya kukagua miradi ya
Mfuko wa Jimbo wilaya za Wete na Chakechake, Pemba.
***********************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amewataka watendaji wa Serikali wanaosimamia miradi
mbalimbali ya maendeleo kuzingatia sheria wanapotekeleza shughuli zao.
Simbachawene ametoa kauli hiyo wilayani Chakechake, Pemba wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya Mfuko wa Jimbo katika
wilaya za Wete na Chakechake kisiwani Pemba.
Alisema kuwa Katika kuhakiksha mfuko unatekelezwa vizuri watendaji hao wana wajibu wa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika hatua zote za utekelezaji wa
miradi ili mwishoni waweze kuandika taarifa.
Akizungumza na wabunge wa majimbo yaliyopo katika wilaya hizo pamoja na watendaji hao alibainisha kuwa nafasi ya mbunge na kamati inayosimamia mradi
kupitia Mfuko wa Jimbo ni kubwa na wanapaswa kufanya kazi hadi kukamilika kwake.
“Wajibu wa kamati unaendelea hadi mradi ukamilike kwani baadaye mtatakiwa kuandika ripoti ya nini kimefanyika tangu mwanzo wa mradi hivyo kukataa kushirikiana na mbunge hakuna tija ni kinyume cha utaratibu na sheria na pia mbunge anapaswa kusimamia mradi kuona kama kuna value for money,” alisisitiza.
Awali wakitoa maoni yao kwa waziri baadhi ya wabunge akiwemo Maida Hamed Abdallah wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba waliomba wawe wanashirikishwa katika kamati za miradi ndani ya majimbo pamoja na kuwa wao
hawana mufuko wa jimbo.
Walisema kuwa kutokana na wao kutokuwa sehemu ya kamati inakuwa ni jambo gumu kuweza kulitolea ufafanuzi wa namna gani fedha za mfuko zimetumika
kwakuwa wanakosa taarifa muhimu.
Miradi aliyotembelea Simbachawene ni mradi wa skuli ya maandalizi Kangagani na mradi wa maji safi na salama Wingwi Mjazana iliyopo Wilaya Wete. Pia alitembelea miradi skuli ya Vikungani na mradi wa umeme wa Pujini iliyopo Wilaya ya Chakechake.,
Waziri Simbachawene katika ziara hiyo pia alitembelea Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu, Unguja ambapo alipata nafasi ya kukutana na baadhi ya watumishi na kusalimiana,