Home Mchanganyiko MAAGIZO 5 YA KATIBU MKUU MWALUKO KWA JUKWAA LA TAIFA LA USIMAMAIZI...

MAAGIZO 5 YA KATIBU MKUU MWALUKO KWA JUKWAA LA TAIFA LA USIMAMAIZI WA MAAFA 

0

*******************************

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko ametoa maagizo 5 kwa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini ili liweze kutoa ushauri wa kitaalamu utakao weza  kupunguza madhara ya maafa na rasilimali zinazohitajika katika upunguzaji wa madhara hayo.

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma tarehe 16 Desemba, 2019, wakati akifungua kikao cha Jukwaa hilo ambapo amebainisha kuwa wakati wa kukabili majanga na maafa kunakuwepo na mipango mingi ambayo hutekelezwa na wadau wa menejimenti ya maafa na kwa uchache wakati wa urejeshaji hali wa maafa,  lakini mipango ya kujiandaa na  kuzuia maafa ambayo hufanyika kabla ya maafa kutokea  kwa ajili ya kuzuia au kupunguza madhara ya  maafa yatakapotokea huwa haitekelezwi.

Jukwaa hilo ambalo linajumuisha wataalamu wa fani mbali mbalimbali  kwa kujumuisha sekta ya umma na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na umoja wa mataifa na asasi za kiraia jukumu lake la  msingi ni kutoa ushauri maeneo ya kipaumbele katika usimamizi wa maafa kwa uratibu na ushirikishawaji wa wadau ili kufanikisha kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango na sera za maendeleo ya taifa na katika misaada ya kibinadamu.