Sehemu ya Wadau kutoka sehemu mbalimbali walioshiriki katika sherehe za maadhimisho ya wiki ya
usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau ulioandaliwa na
Wizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa Landmark jijini Dodoma.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya jinsia Wanawake na Watoto Mh, Ummy Mwalimu , Naibu
Waziri Ofisi ya Maakamu wa Rais- Mh. Mussa Sima pamoja na Viongozi wengine waliohudhuria katika
hafla ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa wakiimba
kwa pamoja wimbo maalum wa Wafanyakazi, mkutano huo uliaandaliwa na Wizara ya Afya jijini
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Maakamu wa Rais- Mh. Mussa Sima akiongea wakati wa maadhimisho ya wiki ya
usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau ulioandaliwa na
Wizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa Landmark jijini Dodoma. Mgeni Rasmi katika Mkutano
huo alikua Waziri wa Afya jinsia Wanawake na Watoto Mh, Ummy Mwalimu.
***************************************
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amezitaka Halmashauri zote nchini kugawa tozo na faini zote zinazopatikana kwenye
mapato ya ndani kuzigawa kulingana na Mpango kazi wa Maafisa Mazingira waliopo kwenye Halmashauri husika.
Alisema hayo wakati alipohudhuria katika maadhimisho
ya wiki ya usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau ulioandaliwa na Wizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa Landmark jijini
Dodoma.
“Mgawanyo lazima uende kwenye usafi na mazingira na mgawanyo ambao hauendi kwenye usafi na mazingira sisi tutambea na kusimamia hili “ alisema Naibu Waziri
Sima.
Aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo yenye jukumu la kulinda, kusimamia na kuhifadhi mazingira na kusisitiza kuwa wapo Maafisa mazingira kuanzia ngazi ya Kijiji na kusisitiza kuhuisha Kamati za Mazingira.
Hivyo amewataka Maafisa Afya kuwa na ushirikiano na Kamati za Mazingira zilizopo kwenye ngazi za chini za Serikali za Vijiji, Kata na Wataalamu wa Mazingira waliopo katika Mikoa na Wilaya.
Akiongea katika warsha hiyo Mh Ummy Mwalimu alisema ni muhimu kuhamasisha vijana kuweza kujenga vyoo bora katika kila kaya kwa ajili ya kuweza kulinda afya na
kuepuka magonjwa mbalimbali na kulinda mazingira.
Amewataka na Halmashauri zote nchini kutimiza wajibu wa kujenga vyoo na kutolea mfano wa Wilaya ya Njombe ambao wamepiga hatua kubwa katika ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya na kuweza kufikia asilimia 96.
“Taarifa ya world bank inaonyesha watu wanapoteza saa 58 kwa mwaka sababu ya kutokua na vyoo . Hivyo basi Wananchi wanatakiwa kufikiria kupoteza hizo saa 58
badala ya kufanya shughuli za kuweza kujiingizia kipato na kuinua uchumu wa Nchi yetu” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy ameunga mkono mapendekezo ya Naibu Waziri Sima katika suala la ushirikiano kati ya Maafisa Afya na Mazingira waliopo katika Halmashauri na miji.