Wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa magari ya kisasa ya mizigo
aina ya Hongyan wakishuhudia moja kati ya magari hayo, kampuni ya MFK Automobile Tanzania
kushirikiana na Hongyan kutoka China walizindua magari hayo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa MFK Automobile Tanzania, Mehboob Karmali (kushoto) akikabidhiwa funguo na
Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong kuashiria uzinduzi wa magari ya
mizigo ya kisasa aina ya Hongyan yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika
Mashariki kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali akizungumza na wageni waalikwa
kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan.
Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong akizungumza na wageni waalikwa
kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan.
Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina
Ngalula akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka
china aina ya Hongyan.
Picha ya pamoja kati ya Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara
maarufu MS. Angelina Ngalula (wa nne kulia) na viongozi wa MFK Automobile Tanzania na SAIV IVECO-
HONGYAN kutoka China kwenye hafla ya uzinduzi wa Hongyan.
*************************************
Dar Es Salaam Tarehe 13 Dec 2019: Kampuni ya MFK Automobile ambayo inajihusisha na uingizaji,
usambazaji na uuzaji wa magari ya mizigo nchini, imezindua magari ya kisasa yenye uwezo wa hali ya juu
na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad
Karmali alisema shukrani za pekee kwenu kwa kuitikia wito wetu wa mualiko wa uzinduzi wa vifaa vipya
vya kampuni ya MFK, Gari ambazo kwa mara ya kwanza kuingia Afrika Mashariki aina ya HONGYAN.
MFK ni kampuni mpya ambayo inajishughulisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari mbalimbali
aina ya Tiper na Tracto head, tumekuja kuunga jitihada za serikali za kuelekea uchumi wa viwanda
ambapo utawezesha fursa mbalimbali katika kukuza uchumi, tutatengeneza fursa kwa wasafiri na
wasafirishaji na ndio sababu kuu iliyotufanya kuleta magari yenye teknolojia ya ulaya na umadhubuti wa
China alisema Karmali.
Katika magari haya ya Hongyan, MFK Automobile inawapa Watanzania bidhaa yenye ubora kwa
mtumiaji na mmiliki,bila usumbufu wowote na kiufundi wa gari hizi za HONGYAN, zina manufaa mengi
kwa mmiliki kwa kumuwezesha kuhimili barabara zozote nchini, matumizi madogo ya mafuta na zina
chumba cha kupumzika kwa dereva aliendelea kusema Karmali.
Pia tumeona fursa katika sekta ya usafiri na usafirishaji, hivyo tumejipanga katika kuleta vifaa vyenye
ubora ambavyo vitahakikisha Tanzania inakuwa kituo kikuu katika sekta hii kwenye ukanda huu wa
Afrika ya mashariki na kati.
“Lengo kuu la kampuni yetu ni kufanya Tanzania ipate bidhaa zenye ubora na za bei nafuu zinazoendana
na kasi ya uchumi wa viwanda ambayo ni moja ya sera ya serikali ya awamu ya tano ili kufikia uchumi
huo wa kati ifikapo mwaka 2025, MFK tunasimamia hilo”, alimalizia kusema Karmali.
Tunajisikia fahari kufanya kazi na kampuni hii ya utengenezaji wa magari,katika ushirikiano huu wa
IVECO GROUP NA WASHIRIKA WAO WA CHINA HONGYAN.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara
maarufu MS. Angelina Ngalula alisema “sekta ya usafirishaji imetoka mbali sana nakumbuka tulianza
tukiwa na malori aina ya Scania 682 hadi kufikia sasa tunatumia magari ya kisasa zaidi, tunawashukuru.
MFK kwa mpango huu wa kuleta magari haya ya kisasa, pia yatatufanya sisi wafanya biashara kuyanunua
kwa umoja wetu tuuweze kufanya sekta hii ya usafirisahji kuwa pana zaidi ukanda huu,. Pia nawaomba
mabenki yaweze kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa sekta hii kwani haina ubabaishaji kurudisha
mikopo hiyo. alisema Ngalula.
Aliongezea kusema Ngalula “tuna bidhaa nyingi sana zinahitaji usafirishaji kama vile mazao, shaba,
madini mbalimbali, hii itasaidia kuweka vituo vya kufanyia huduma(service) za magari na kuuza vipuri
mikoani ili kuepusha wizi unaotokana na madereva wasio waaminifu”.
Hata standard gauge SGR itahitaji zaidi kushirikiana na sekta hii ya usafirishaji ili kuwafikishia mizigo kwa
urahisi zaidi, huwezi kuwa na Treni bila kuwa na magari ya mizigo, ukizingatia usafirishaji wa kutumia
barabara unahitajika kwa asilimia 75 . alimalizia kusema Ngalula.
Nae Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, -MS Winnie Xiong alisema hii ni fursa ya
kipekee kwa kampuni yetu kuleta magari haya nchini Tanzania, hasa ukizingatia Tanzania na china
zimeweka mahusiano ya kidiplomasia miaka 55 hadi sasa tokea mwezi Aprili 26, 1964, nchi hizi mbili
zimejenga uhusiano imara na kushirikiana bega kwa bega. Leo nawaahidi kuwa Hongyan itazalisha
magari bora ya mizigo kwa soko la Tanzania kwa kupitia washirika wetu MFK na kuwawezesha wateja
wetu kugharamia huduma na vipuri vya magari haya kwa bei nafuu. alimaliza kusema Xiong.