Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom wakiwa wamebeba bango lenye picha ya simu ya Smart Kitochi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jijini Mwanza.
Kaimu mkuu wa mauzo wa Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu ya Smart Kitochi, uliofanyika jijini Mwanza.
Wateja wa simu mpya za Smart Kitochi zenye uwezo wa 4G kutoka Vodacom wakipatiwa maelezo ya kuhusu simu hizo zitakazopatikana kwenye maduka ya Vodacom nchini kote kwa bei ya shilingi 45,000/= katika msimu huu wa sikukuu wakati wa uzinduzi wa simu hizo jijini Mwanza.
Wateja wa simu mpya za Smart Kitochi zenye uwezo wa 4G kutoka Vodacom, wakijipiga selfie kwa kutumia simu hiyo baada ya kuinunua jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo inayopatikana kwenye maduka ya Vodacom nchini kote kwa bei ya shilingi 45,000/= katika msimu huu wa sikukuu.