Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akifungua eneo lililowekwa jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa FETA Kampasi ya Mikindani, Mkoani Mtwara.
Baadhi ya wahitimu wa kozi fupi za ufugaji samaki wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ufunguzi wa FETA Kampasi ya Mikindani, Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa tatu kutoka kulia) akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa FETA Kampasi ya Mikindani, Mkoani Mtwara
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wahitimu wa kazo fupi za ufugaji samaki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa FETA Kampasi ya Mikiandani, Mkoani Mtwara.
*********************************
Na. Edward Kondela
Serikali imesema inahakikisha sera yake ya kuhamasisha wananchi kufuga samaki inatekelezwa kote nchini ili kutosheleza mahitaji ya soko la samaki nchini pamoja na kukuza pato la taifa na mtu mmoja mmoja.
Akizungumza Mjini Mtwara, wakati akifungua tawi la Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameiagiza FETA kwa kushirikiana na Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji kutoka katika wizara hiyo, kuandaa mitaala ya ufugaji viumbe kwenye maji wakiwemo samaki, kaa, majongoo bahari na Kambakochi kwa ajili ya wananchi wa Ukanda wa Pwani ili waweze kuongeza vipato vyao kupitia fursa ya ufugaji. PAUSE
Mhe. Abdallah Ulega – Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi
Aidha Mhe. Ulega ameagiza uundwaji wa vikundi vya uzalishaji kaa, Kambakochi, majongoo bahari pamoja na wazalishaji wa zao la mwani ili iwe rahisi kwa vikundi hivyo kutambulika rasmi pindi mazao yao yanapohitajika sokoni, na watu waweze kufika katika mashamba yao ya ufugaji kwa ajili ya kuvua samaki na viumbe vingine wakiwemo kaa, kambakochi na majongoo bahari ambao wamekuwa na soko kubwa sana na mahitaji yake kuongezeka katika baadhi ya maeneo zikiwemo hoteli za kitalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka FETA Bw. Ambakisye Simtoe amesema chuo hicho kimepanga kuzalisha wagani kwa ajili ya kuendeleza na kukuza tasnia ya uvuvi nchini pamoja na kununua mashine ya kuzalisha vifaranga bora ili iwe rahisi kwa wananchi wa Ukanda wa Pwani kupata vifaranga hivyo kwa bei nafuu huku katika risala ya wanafunzi hao wakisema mafunzo waliyoyapata yakiwemo ya ufugaji wa samaki yatawawezesha kujiajiri. VOX
Bw. Ambakisye Simtoe – Mkurugenzi wa Mafunzo FETA
Bi. Monica Mfaume – Msoma risala kwa niaba ya wanafunzi
Jumla ya wanafunzi 62 wamehitimu kozi fupi ya ufugaji samaki katika chuo cha FETA Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara na kukabidhiwa vyeti na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ambaye amekifungua rasmi chuo hicho chenye uwezo wa kudahili wanafunzi 240 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mahitaji ya soko la samaki nchini ni Tani 700,000 hadi 800,000 kwa mwaka huku uzalishaji ukiwa wastani wa Tani 400,000 hadi 450,000 hali ambayo Naibu Waziri Ulega amesisitiza kwa chuo cha FETA Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara kuwa kampasi ya mfano katika kutoa mafunzo ya ufugaji samaki, kaa, kambakochi na majongoo bahari ili wananchi waweze kutosheleza soko la ndani na kukuza vipato vyao na taifa kwa ujumla.