Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Bernard Konga akiongea na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kutumia vyombo vyao vya habari kuwaeleza wananchi faida za kujiunga na vifurushi vipya kwani vimezingatia makundi yote katika jamii kwa lengo la kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa huduma ya matibabu. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF)Bw. Christopher Mapunda akiongea na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo alisema kuwa viwango katika
vifurushi vya bima ya afya sio gharama za matibabu bali ni uchangiaji ndio maana hata ukiumwa na kutumia zaidi ya kiwango cha laki moja na tisini na mbili, mfuko utagharamikia matitabu hayo. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Hipoliti Lello na akitoa mada kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo aliwaeleza kuwa mpango wa
vifurushi sio mpya na NHIF imeanzisha mpango huo kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi kulingana na mahitaji yao. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya.
wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakifuatilia uwasilishaji wa mada kutoka kwa wataalam wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF), Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
**************************
Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Umewapiga Msasa wanahabari Mkoa wa Mbeya kuhusu Vifurushi vya Bima ya Afya na kuwasisitiza kutumia kalamu zao kuwaeleza wananchi umuhimu wa kujiunga ili kuwa na uhakika wa matibabu.