Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameketi na
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ndani ya ndege mpya iliyonunuliwa na Serikali aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mara baada ya kuwasili.
Picha mbalimbali zikionesha Ndege hiyo ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati ikitokea nchini Canada.
Ndege mpya aina ya DE Havilland DASH8-400 ikipokelewa
kwa saluti ya maji na Kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ilipotua Uwanja wa Ndege wa Mwanza ikitokea Canada na kupokelewa na maelfu ya watu wakingozana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli Jumamosi Desemba 14, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donell na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuipokea rasmi ndege mpya ya DE Havilland DASH8-400
katika uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumamosi Desemba 14, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapongeza kwa furaha marubani wazalendo walioendesha ndege mpya ya DE Havilland DASH8-400
kutoka Canada na kutua salama katika uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumamosi Desemba 14, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa ATCL wakati wa mapokezi ya ndege mpya ya DE Havilland DASH8-400 kutoka Canada na kutua salama katika uwanja
wa Ndege wa Mwanza Jumamosi Desemba 14, 2019.
PICHA NA IKULU