Na Mwandishi Wetu.
ALIYEKUWA Katibu wa Baraza la Wazee la klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Ibrahim Omary Akilimali amefariki dunia Alfajiri ya leo Bagamoyo mkoani Pwani.
Taarifa ya klabu ya Yanga SC leo imesema kwamba mazishi ya Mzee Akilimali yanatarajiwa kufanyika kesho Saa 10:00 jioni makaburi ya kwa Mtogolwe, Tandale Jijini Dar es Salaam.
Akilimali ambaye ni mzaliwa wa Kigoma amekuwa mpenzi wa Yanga tangu mwaka 1956, ushabiki aliorithi kwa marehemu yake na wote waliipenda klabu hiyo wakiamini ni ya wazalendo.

Upenzi wake kwa Yanga ulizidi zaidi baada ya kuhamia Dar es Salaam mwaka 1966 kabla ya mwaka 1967 kuajiriwa kama mmoja wa wabeba mizigo wa Bandarini, maarufu kama Kuli.
Alipata kadi yake ya kwanza ya uanachama wa Yanga mwaka 1972 na amewahi kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo kabla ya uteuzi wake katika Baraza la Wazee la klabu.
Akilimali ambaye pia alikuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), atakumbukwa kwa misimamo yake zaidi ya kuitetea Yanga isimame kama ilivyo na si kuchukuliwa na watu kwa kofia za ukodishaji, au uwekezaji akipendekeza zaidi mfumo wa hisa.
Mungu ampumzishe kwa amani Mzee Akilimali. Amin.