Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma akiingia katika viwanja vya Shule ya Sheria kwa vitendo (School of Law) kwa ajili ya kuwapokea na kuwakubali Mawakili wapya wapatao 558 ikiwa ni sherehe ya 61.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe.Sharmillah Sarwatt akitaja majina ya Mawakili wapya waliokubaliwa na kuapishwa leo katika katika viwanja vya Shule ya Sheria kwa vitendo (School of Law).
Mawakili wapya waliokubaliwa na kuapishwa leo wakitoa heshima kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria kwa Vitendo wakifuatlia sherehe ya kuapishwa Mawakili hao.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi (watatu kushoto)wakiwa na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiinama kwa ajili ya kuwapokea na kuwakubali Mawakili hao.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kushoto) wakiwa na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakifuatilia sherehe hiyo.
aji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kushoto) wakiwa na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwakubali na kuwapokea Mawakili hao.
…………………
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewashauri Mawakili wapya kutumia elimu ya sheria kibiashara ili kuweza kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira katika sekta hiyo.
Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 13, 2019 katika mahafali ya 61 ya kuwapokea na kuwakubali Mawakili wapya 558 yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sheria kwa Vitendo (School of Law) jijini Dar es Salaam.
Ambapo alisema sekta hiyo, katika karne ya 21 inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni shinikizo la kiuchumi, kijamii na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Alisema uzoefu wa huko Marekani katika kukabiliana na changamoto ya Mawakili kukosa ajira ni kuwapatia elimu maalum ya biashara, na mbinu za kufanya biashara.
“Mawakili lazima watambue Makampuni yao ya Uwakili (Law Firms) ni biashara kama zilivyo biashara zingine. Ujuzi wa biashara utamwezesha Wakili afahamu biashara ya Kampuni yake ya Uwakili. ujuzi wa biashara ni zana ya kuendeshea Kampuni yako ya Uwakili au biashara nyingine yoyote ile”, alisema Jaji Mkuu.
Aidha, alisema kuwa ujuzi katika biashara utawaweka katika hali ya utayari wa kushidana katika soko la huduma ya uwakili katika dunia ambayo mipaka ya huduma hizo na zinginezo zenye ushindani mkubwa.
Aliongeza kuwa changamoto ya Mawakili kukosa ajira za kudumu ipo katika nchi nyingi kama vile Australia, Marekani, na Kanada.
“Mawakili lazima mkubali ushindani kutoka nje ya Tanzania. Jengeni madaraja ya ushirikiano na Mawakili wenzenu vijana wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili mtafute biashara ndani na nje ya Tanzania”, alisisitiza.
Aliongeza kwamba mawakili hao, wanapaswa kujifunza lugha za kimataifa kwa ufasaha mfano:- Kiingereza, Kifaransa na Kichina.
Naye Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius Njole amewashauri, kuwa kwenda kufanya kazi katika maeneo yaliyo mbali na miji mikubwa yakiwemo maeneo ya vijijini kwa kuwa yana uhitaji mkubwa wa huduma hizo.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dkt. Rugemeleza Nshala aliwasii wafanye kazi za uwakili kwa bidii, weledi na kuzingatia maadili ili kuiwezesha Mahakama kutimiza jukumu la msingi la kutenda haki.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma hapa Tanzania inaonyesha kuwa ni idadi ndogo ya wahitimu wa Sheria walioomba kujaza nafasi za kazi katika Utumishi wa Umma ndio walifanikiwa kupata ajira 2017/2018, ambapo walioomba walikuwa 3,250 waliopata walikuwa 88 sawa na asilimia 2.7na mwaka 2018/22019 walioomba walikuwa 2,826 waliopata walikuwa 19 sawa na asilimia 0.6.