Home Mchanganyiko WAZIRI KAMWELWE AONGOZA MKUTANO WA ...

WAZIRI KAMWELWE AONGOZA MKUTANO WA 13 WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TANROAD TAIFA, KAGERA.

0

Na Silvia Mchruza.Kagera.  

Mkutano wa 13 wa baraza la wafanyakazi wa tanroad taifa kwa mala ya kwanza umefanyika mkoani kagera ukiongozwa na wazili wa uchukuzi na ujenzi   Isack  Kamwelwe  katika ukumbi wa  ELCT manispaa  ya Bukoba.

Baraza hilo lililoudhuriwa na wajumbe tofauti tofauti kutoka mikoa yote nchini pamoja na mkuu wa mkoa wa kagera Brigedia General Erisha Marko Gaguti sambamba  na mwenyekiti wa baraza hilo ambae pia n I mtendaji mkuu wa Tanroad Taifa Patrick  Mfugare ikiwa lengo kuu la kufanyika  kwa baraza hilo ilikuwa ni kujadili maadhimio yaliyopatikana  katika baraza lilopita pamoja na kutatua changamoto hizo katika mwaka wa fedha 2018/19.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo waziri Kamwelwe amesema kuwa  Tanroad ndiyo kwa upande m wingine ni muhimili wa taifa kutokana na kazi wanazofanya za kujenga taifa kupitia maendeleo ya barabara zinazojengwa na miradi mingine mikubwa ambayo pia inawanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.

“Lakini nitoe rai kwa watanzania wenzangu maana sisis wenyewe watanzania tunazungukana ila tu naamini watu wa hivyo tutawapigia kwata za kimyakimya wale wote wanaokwamisha maendeleo ya Tanroad na taifa kwa ujumla lazima tu tutawabaini.”alisema waziri Kamwelwe.

Aidha ameongeza kuwa serikali hii ya awamu ya tano aijawaangusha watanzania kutokana na kutekeleza miradi mikubwa kwa midogo ambayo inaonekana wazi kwa wananchi woteikiwa ipo chini ya Tanroad,pia amesema kuwa amefurahishwa na utekelezwaji wa maagizo yake aliyoyatoa katika mkutano wa 12 wa baraza lililopita.

“Pia  niendelee kuwasihii na kuwatia moyo kuendelea kutanguliza maslai ya taifa na wananchi kwa ujumla huku serikali ikiendelea kutatua kero ambazo zinzweza kukwamisha utekelezaji wenu “

Sambambamba na hayo waziri kamwelwe ameongeza kuwa licha kutekeleza miradi yao wasikibali kuingiliwa katka majukumu yao na kujitaidi kutafuta mbinu ya kuzuia utovu wa kwa watu wanaokwamisha maendeleo ya Tanroad huku akimalizia kwa kumuagiza meneja wa tanroad Kagera kuhakikisha anamfuatilia mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya nyakanazi mkoani kagera wilaya ya Biharamulo uishe mala moja kabla ya uchaguzi.