Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji Silvestry Koka akifafanua jambo kwa wajumbe 94 hawapo pichani wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji katika eneo la kibamba CCM wakati wa ziara ya kugagua mradi wa kimkakati wa ujenzi wa upanuzi wa barabara ya njia nane ya morogoro kutokea kimara hadi Kibaha,yenye urefu wa kilometa 19.2 (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mwakilishi wa Meneja kutoka Wakala wa (TANRODS) Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Issa Mbura wa kulia akiwa akimpa maelezo ya mradi wa ujenzi wa upanua wa barabara ya njia nane eneo la Kibamba Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji Silvestry Koka kushoto mara baada ya wajumbe hao walipofika kuijinea shughuli zinazoendelea.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji Silvestry Koka kushoto akifafanua jambo kwa Mwakilishi wa Tanrods Mkoa wa Dar es Salaam Issa Mbura wakati wa ziara hiyo ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji jinsi ya mwenendo mzima wa jinsi ya ujenzi unavyoendelea(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Wajumbe wapatao 94 wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yao ya kujionea mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa upanuzi barabara ya njia nane ambayo inatokea kimara hadi Kibaha ambayo inajengwa na serikali kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
**********************************
VICTOR MASANGU,KIBAHA
MRADI mkubwa wa kimkakati upanuzi wa njia nane wa barabara ya morogoro kutokea kimara hadi Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2 licha ya kufikia kiwango cha asilimia 59.1 hadi sasa ya ujenzi wake lakini imeelezwa bado ulikuwa unakabiliwa na changamoto ya kukwama katika baadhi ya maeneo kutokana na kuwepo kwa mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha hivi karibuni hivyo kupelekea miundombinu mingine kuharibika.
Hayo yalibainishwa na mwakilishi kutoka Wakala wa (TANRODS) Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Issa Mbura wakati wa ziara ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji ambao wametembelea mradi wa huo ambao umefikia maeneo ya kibamba kwa lengo na kukagua miradi mbali mbali ya kimikakati ya serikali ikiwa ni moja ya kujionea utekelezaji wa ilani ya chama jinsi inavyokwenda kama maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli yalivyotolewa.
Kwa upande wake Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka alimpongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kwa ujenzi wa upanuzi huo wa barabara ambao utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kibaha pamoja na Taifa kwa ujumla kwani utasaidia kuleta chachu ya kimaendeleo na kuondokana na kero kubwa ya msongamano wa magari ambao umekuwa unakwamisha shughuli mbali mbali za ujenzi wa Taifa kutokana na kupoteza muda mwingi njiani.
Aidha Koka aliiomba serikali ya awamu ya tano kuendelea kuiboresha miundombinu ya barabara ikiwemo kufanya upanuzi amabao utasaidia kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo amabayo yamekuwa ni kero kubwa hivyo kukamilika kwa mradi huo utaleta unafuu hata kwa wananchi ambao walikuwa wanasafiri kwa usafiri binafisi.
“Ofisi ya Mbunge kwa kushirikioa ana wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) katika KIbaha mji tumeona ni vema tufanye ziara maalumu kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya mikakati ambayo ipo katika utekelezaji wa ilani ya chama, lengo ikiwa ni kuona mambo jinsi yanavyokenda, lakini kikubwa namshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha ambazo kwa sasa tunajionea matunda yake katika nyaja tofauti,”alisema Koka.
Aidha mwakilishi huyo wa Tanrods akifafanua zaidi amesema kwamba mradi huo utakwenda wa awamu mbali mbali ambapo baada ya kukamilika mpaka Kibaha utaendelea katika mikoa mingine ya Morogoro hadi makao makuu ya nchi Dodoma lengo ikiwa ni kuzipanua barabara hizo ambazo zitasaidia kurahisiha magari kufanya safari zake kwa urahisi.
“Kwa sasa mradi huu tunaendelea nao vizuri lakini kikubwa hapa tunaendelea na ujenzi na kwa faida ya wananchi wote mradi huu kwa sasa utekelezaji wake upo katika awamu ya kwanza, na vile vile utaendelea katika awamu nyingine hadi Mkoani Dododoma kulingana na bajeti ya fedha ambayo itakuwa ikipatikana na ujenzi huu ukikamilika utakuwa ni msaada wa kupunguza sana msongamano,”alisema.
ZIARA hiyo ya wajumbe 94 wa halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha Mji kutoka kata zote 14 imetembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ile ya kimikakati saba ambayo inatekelezwa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo katika sekta, afya, maji , elimu,soko, pamoja na miundombinu ya barabara,kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.