Mkurugenzi wa huduma za Elimu -CSSC Mwl.Petro Masatu ,akisoma Risala kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa pili wa walimu wakuu wa shule za awali na za msingi za makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] ulifanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI] Dkt.George Jidamva,akifungua mkutano wa pili wa walimu wakuu wa shule za awali na za msingi za makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] kwa niaba ya Naibu katibu mkuu TAMISEMI Gerald Mweli aliyemuwakilisha uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa pili wa walimu wakuu wa shule za awali na za msingi za makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi uliofanyika jijini Dodoma.
Mshauri wa huduma za elimu CSSC ,Joshua Moshi,akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa pili wa walimu wakuu wa shule za awali na za msingi za makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] ulifanyika jijini Dodoma.
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
TUME ya Kikristo ya Huduma za Jamii(CSSC), imeiomba serikali kuondoa leseni ya biashara kwenye vyuo na shule zinazomilikiwa na taasisi za dini kwa kuwa elimu wanayotoa ni hisani na sio biashara.
Raia hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa huduma za elimu wa tume hiyo, Mwalimu Petro Masatu katika ufunguzi wa mkutano wa pili wa walimu wakuu wa shule za awali na za msingi za makanisa kilichofanyika jijini Dodoma.
Masatu alisema kuwa baadhi ya halmashauri zimekuwa zikidai leseni wakati taasisi hizo hazifanyi biashara bali zinatoa huduma ya elimu kuisadia serikali kufikisha huduma kwa jamii.
“Tunaomba Ofisi ya Tamisemi ishirikiane na mamlaka zingine kusaidia halmashauri zisidai leseni hizo, shule zetu pia zinatakiwa kulipia gharama za uendeshaji wa shule([WCF) kwa watumishi ipo juu kwa waendeshaji wa shule zetu tunaomba ifanane na serikali, maana kule wanalipa asilimia 0.5 sisi tunalipa asilimia moja, ” alisema.Masatu
Mwalimu Masatu alisema kuwa Tume inaendesha taasisi za elimu 1033 ikiwemo elimu ya awali, msingi, sekondari, seminari, ufundi stadi, ualimu na elimu ya juu na kwa upande wa ufaulu kwa shule za kanisa umekuwa chachu nchini ambapo mwaka 2019 shule zetu zimefaulisha wanafunzi wa Darasa la saba kwa wastani wa A na B hivyo vijana wote wataingia kidato cha kwanza mwaka 2020.
Masatu alisema tume imeanzisha mitihani ya pamoja kwa wanafunzi wenye mitihani ya kitaifa kabla ya kufanya mtihani wa taifa ili kufanya ulinganifu wa mitihani hiyo.
Akifungua mkutano huo,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Elimu, Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala wa ofisi hiyo, Dk.George Jidamva, alisema shule za kanisa ndio zimekuwa kimbilio kwa kuwa ufaulu mkubwa na ongezeko la ufaulu linachangiwa na shule hizo.
“Serikali inatambua jitiuhada zote zinazofanywa na kanisa na taasisi zake katika kujenga elimu ya Tanzania tusingependa sana wadau wetu wanaosaidia kuelimisha mkawa mnanung’unika, “alisema Jidamva
Aidha aliwashauri kuwasilisha changamoto wanazopata na zile ambazo zipo nje ya mamlaka ya Tamisemi ili kuangalia namna ya kuzihusisha wizara zingine na kutafutiwa ufumbuzi.
“Kuhusu leseni, ni utaratibu wa kawaida wa serikali kwa mtu yeyote anayefanya shughuli za kujiingizia kipato, napenda hilo tulipate kwa upana wake, tunakwazika na nini linapokuja suala la leseni tutaangalia namna ya kulifikisha kwenye mamlaka husika,”alisisitiza Jidamva
Alifafanua kuwa hili la asilimia moja ya WCF ni mambo ya kukubaliana yanahitaji mazungumzo ya pamoja ni namna gani hiyo WCF inaweza kulingana na serikali, ni mambo gani kanisa litapoteza au kunufaika, liandikwe kwa lugha ya kitaalam ili lipitishwe kwa wataaalam wetu waweze kushauri mamlaka husika.