Home Biashara VETA yatoa gawio la Shilingi Bilioni 1 kwa Serikali

VETA yatoa gawio la Shilingi Bilioni 1 kwa Serikali

0

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya Shilingi bilioni moja kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ndg. Peter Maduki (kushoto) ikiwa ni gawio la VETA kwa Serikali katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma leo tarehe 12 Desemba 2019. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu. Wengine katika picha ni Msajili Hazina, Athumani Mbuttuka na Naibu Katibu Mkuu, Adolf Ndunguru.

Watendaji Wakuu wa VETA wakisikiliza nasaha kutoka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati wa hafla ya kuwasilisha gawio kwa Serikali iliyofanyika jijini Dodoma leo, tarehe 12 Desemba 2019. Katika hafla hiyo VETA imetoa gawio la Shilingi Bilioni Moja. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Ndg. Peter Maduki, Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa VETA Ndg. Anthony Kasore (kushoto).