Home Mchanganyiko MRUNDIKANO WA WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI BADO CHANGAMOTO NCHINI

MRUNDIKANO WA WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI BADO CHANGAMOTO NCHINI

0

Mkurugenzi Msaidizi Uendeshaji wa Sera kutoka wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,akimuwakilisha Naibu katibu wizara hiyo Dkt.Avemaria  Semakafu,akifungua kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Children in Crossfire Craig Ferla akizungumzia mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu kwa madarasa ya awali shule za serikali unaotarajiwa kuanza utekelezaji wake mkoani Dodoma mwezi Januari 2020

Mwakilishi wa Kamishina wa Elimu  Waziri ya Elimu Sayansi na Teknologia,kutoka kitengo cha mafunzo ya Ualimu Bi.Naomi Swai,akiongoza mjadala kwenye kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Mtafiti mwandamizi wa kimataifa kutoka taasisi ya Mathematica inayojishughulisha na masuala ya utafiti , Candace Miller,akiwasilisha matokeo ya utafiti uliotokana na mradi wa fursa kwa watoto uliotekelezwa na mashirika ya TAHEA Mwanza, Childhood Development Organisation, Aga Khan University na kuratibiwa na Children in Crossfire, unaitwa Fursa kwa Watoto

Afisa Mafunzo kutoka Add-International Bw.Japhari Shehanghilo,akitoa hoja katika kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Mwalimu kutoka chuo cha Ualimu Butimba TC kilichopo jijini Mwanza,Modesta Ng’aida,akisisitiza jambo katika kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Mwalimu wa darasa la awali shule ya msingi Madizini wilayani Mvomero Mkoani Morogoro ,Monica Kibena,akichangia mada katika kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Mtaalamu wa masuala ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudhumia Watoto,(UNICEF) Tanzania,Bw.Karam Ali,akitoa maada  katika kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Sehemu ya wataalamu wa Elimu kutoka sehemu mbalimbali katika kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifatilia maada mbalimbali katika kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

Afisa Elimu kutoka wizara ya Elimu Makao Makuu,Bw.Clement Mswanyama,akitoa muongoza kwa washiriki wa kikao cha wataalam wa Elimu Ulioandaliwa na Serikali kupitia  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu ya awali jijini Dodoma

…………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Wadau mbalimbali wa elimu ya awali nchini wamesema mrudindikano wa wanafunzi wa darasa la awali umeelezwa kuwa changamoto kwa wanafunzi wa darasa hilo hali inayowafanya walimu kushindwa kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja katika ufundishaji.

Wamesema hayo wakati wakizungumza Jijini Dodoma jana wakati wa mkutano uliowaandaliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekonolojia pamoja na Tamisemi ukiwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu ya awali wakiwemo asasi za kiraia, vyuo vikuu na waalimu.

Mmoja wa wachangiaji katika mkutano huo, Mwalimu wa darasa hilo katika shule ya msingi Madizini wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Monica Kibena alisema, madarasa wanayofundisha yana wanafunzi kuanzia wanafunzi 150 hadi 200 ambao alisema ni mwalimu mmoja hawezi kulimudu darasa .

Kibena alisema,mrundikano huo unawafanya walimu kushindwa kufanya upimaji wa mtoto mmoja mmoja ili kujua uelewa, hivyo ili kuikabili changamoto ni vyema Serikali ijenge madarasa ya kutosha na kuwagawangwa wanafunzi hao kwa uwiano unaotakiwa wa wanafunzi 25 kwa mwalimu mmoja.

“Kwa kweli mrundikano wa wanafunzi wa darasa la awali bado ni changamoto kubwa kwetu,wanafunzi wengi sana hatua inayowafanya walimu wengi kushindwa kulimudu darasa kwa wanafunzi wa darasa hilo wanapaswa kufikiwa mmoja mmoja ili kujua uelewa wake kwani ndio msingi wake…,

“Au Serikali iajiri walimu wengi wa darasa la awali ili darasa moja lifundishwe na mwalimu zaidi ya mmoja.”alisema mwalimu Kibena.

Mwalimu Kibena alitumia fursa hiyo pia kuishauri Serikali kuwatumia baadhi ya walimu waliopata mafunzo akiwemo yeye kutoka CIC ambayo yamewezesha kulimudu darasa kubwa .

Hata hivyo aliwataka walimu wenzake kuwa wabunifu kwa kutafuta zana za kufundishia kulingana na mazingira ili kuongeza uelewa wa wanafunzi wanapokuwa shuleni.

Mkurugenzi Mkazi wa shirika linaloshughulika na masuala  ya makuzi na malezi ya awali ya watoto wadogo (CIC) Craig Ferla alisema ,wadau wa elimu wanapaswa kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za elimu ya awali nchini kulingana na ongezeko la watoto hao.

Alisema,uandikishaji wa watoto kwa mwaka 2016 umeongezeka hadi kufikia 1.5 milioni kutoka watoto milioni moja mwaka 2015.

“Zipo changamoto nyingi katika elimu inayotolewa nchini ikiwemo ya awali hasa katika madarasa hayatoshi hivyo kusababisha kuwepo kwa mlundikano wa wafanzi,  ili kukabiliana nayo ni lazima wadau wote wa elimu washiriki na si kuiachia serikali peke yake,” alisema Ferla.

Hata hivyo amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye utoaji wa elimu bora nchini wamejipanga kuzindua mradi wa elimu ya awali katika mkoa wa Dodoma mwaka 2020 ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Kongwa pamoja na Chamwino na baadae kuenea mkoa mzima .

Amesema mradi huo unalenga kujenga uwezo wa watendaji wakiwemo waalimu wanaofundisha elimu ya awali, wathibiti wa ubora na maofisa elimu katika wilaya za mkoa husika.

Naye Hawa Juma kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa huku akisema Serikali itaifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Hata hivyo alisema,changamoto hiyo inatokana na mafanikio ya Serikali ya wamu ya tano ya mpango wa elimu bila malipo ambapo wazazi wengi wamejitokez kuandikisha watoto katika darasa la awali.

Akifungua Kikao hicho kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Elimu Avemaria Semakafu, Mkurugenzi Msaidizi Uendeshaji wa Sera wa wizara hiyo Bw.Yesse Kanyuma aliipongeza Asasi ya CIC kwa kuanzisha mradi huo ambao unawajengea watoto umahiri pamoja na kutoa mbinu za ufundishaji wa watoto wa darasa la awali.

“Nimeambiwa kuwa shirika hili limekuwa likitekelza programu za watoto hapa nchini kwa ufanisi tangu mwaka 2009 katika mikoa ya Kilimanjaro ,Mwanza na Morogoro .