Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitafakari wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia korosho Nangurukuru wakati alipofanya ziara Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Sehemu ya wakulima na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama wakati alipofanya ziara Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Pwani na Lindi

Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 10 na 11 Disemba 2019 amefanya ziara
ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kilwa mkoani
Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa
mwaka 2018/2019.

Katika
ziara hiyo Waziri Hasunga amebaini baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao jambo
ambalo limemshangaza Kwakuwa serikali ilishatoa fedha zote kwa ajili ya
kuwalipa wakulima.

Amesema
kuwa baada ya ziara ya kikazi katika mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara kubaini
kadhia iliyopelekea kutolipwa fedha hizo serikali itachukua hatua za haraka.

“Sikutegemea
hata siku moja kwamba eti itafika mpaka mwezi wa 12 wakulima wakiwa hawajalipwa
kwakuwa imetokea niwahakikishie wakulima wote ambao walileta korosho zao na
zilipokelewa, wote watalipwa” Alisisitiza Mhe Hasunga

kuwa wapo baadhi ya wakulima ambao wanasema hawajalipwa jambo ambalo sio kweli
kwani wanafanya hivyo ili kukwepa madeni waliyokopa.

Kuhusu
vibarua waliofanya kazi katika msimu huo wa korosho wa mwaka 2018/2019 Waziri
Hasunga amesema kuwa madeni yote halali yatalipwa kwa wakati.

Hata
hivyo ameeleza kuwa katika msimu wa mwaka 2019/2020 serikali haitajiingiza
kwenye ununuzi wa zao la korosho badala yake imetoa fursa kwa wafanyabiashara
kununua korosho.

Sambamba
na hayo pia amesema kuwa serikali inaendelea kujipanga vyema ili katika siku za
hivi karibuni serikali isipange bei elekezi badala isalie kuwa msimamizi mkuu
kuhakikisha haki inatendeka katika biashara hiyo.

Ziara ya
siku moja mkoani Pwani imetoa taswira ya muendelezo wa ziara ya Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambapo leo tarehe 11 Disemba 2019 amewasili katika
mkoa wa Lindi.