**************************
Mh.Dkt.Faustine Ndugulile (Mb) Kigamboni na (NW) @wizara_afyatz ameanza rasmi ziara yake kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake kwa kuanza na kata ya Pembamnazi,Katika ziara hii Mh.Ndugulile ameongozana na Maafisa mbalimbali kutoka Manispaa ya Kigamboni wakiwemo Aron Joshua (A.Mifugo),Kayoza W.Yasintha (A.Elimu Sekondari),Hellen Peter (A.Elimu Ufundi),Catherine Mashalla (A.Elimu msingi),Zacharia Hegga (Mhandisi Ujenzi),Rajab Gundumu (Mchumi) pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Evarist Mruge (Katibu CCM wilaya ya Kigamboni) na Mwenezi wake Ndg.Abdallah Pazi,Mh.Diwani,Mtendaji kata,watendaji mitaa na wenyeviti wa mitaa kata ya Pembamnazi .
Katika ziara hii Mh.Ndugulile amekagua kuhusiana na fedha kutoka mfuko wa jimbo alizotoa kwa ajili ya ukarabati wa sekondari ya Pembamnazi na namna ilivyotumika,Kuhusiana na Ujenzi wa soko la samaki ambapo zilitengwa fedha zaidi ya Milioni 70,pamoja naa ukaguzi wa Miradi ya REA ya umeme kuona kazi iliyofanyika hadi sasa na kutambua changamoto zinazojitokeza ilikusudi kufanyiwa utatuzi kwa haraka .
Katika Maelezo yake Mh.Ndugulile amewataka wenyeviti haswa wapya kufanya kazi kwa ushirikiano…” Ushirikiano..tunataka ushirikiano kutoka kwenu wenyeviti sisi tunatembea kama mnyororo wa baiskeli pingili moja ikikatika kazi inayumba,tunategemea mwenyekiti ufanye makubwa katika mtaa wako itasaidia Diwani kufanya nae makubwa katika kata yake na itanisaidia mimi Mbunge kufanya makubwa katika jimbo langu nami nitamsaidia Mh.Rais wetu kufanya makubwa zaidi mazuri katika nchi yetu…Mimi sitegemei kuona Rais aje atatue matatizo ya Kigamboni maana yake mimi nitakuwa nimeshindwa kazi hivyo lazima nifanye kazi ” Alisema Mh.Ndugulile.
Mh.Ndugulile ametoa wiki mbili (02) kukamilika kwa mradi wa maji katika shule ya msingi ya pembamnazi pia amewataka Maafis Elimu kusimamia vizuri pesa zinazotolewa kwa ajili ya ukarabati katika mashule .
Aidha Mh.Ndugulile amewataka Tanesco kuhakikisha wanashirikiana kupeana taarifa za utekekezaji wa mradi wa umeme kwa viongozi wa kata na mitaa husika.
Mh.Ndugulile amemalizia kwa kuwataka kuwajili vijana kutoka UVCCM katika fursa zote za ujenzi katika utekelezaji wa miradi hii ndani ya jimbo lake la kigamboni .