Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina shabani,akimkabidhi tuzo ya Uandaaji bora wa hesabu za fedha, Afisa Mwandamizi wa TBL,Mahsen Zahoro, kwa niaba ya kampuni wakati wa hafla ya Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) iliyofanyika Bunju, Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki,wengine pichani na wafanyakazi wa TBL kutoka idara ya fedha
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited, imeshinda tuzo ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu mwaka 2018, kukidhi viwango vya kimataifa, imeshika nafasi ya pili katika sekta ya viwanda katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni wa heshima katika hafla hiyo ambayo hutayarishwa na Bodi ya Uhasibu na ukaguzi wa hesabu nchini (NBAA) alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mipango,Amina Shabani.
Akiongelea mafanikIo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Philip Redman alisema “mwaka 2019 umekuwa mzuri na wa mafanikio makubwa kwa kampuni yetu, tumeweza kushinda tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi, hii inadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi ya uendeshaji viwanda kitaalamu nchini.Nawapongeza wafanyakazi wote wa kampuni kwa mchango wao mkubwa katika kupatikana kwa mafanikio haya”.
Redman, alibainisha kuwa mwaka huu kampuni imeshinda tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora mwezi Oktoba na hivi karibuni ilipata tuzo ya kimataifa yak Mwajiri bora ikiwa ni mwaka wa tatu kupata tuzo hiyo mfululizo pia ni moja ya kampuni inayoshikilia rekodi ya kuwa mwajiri bora inayotambuliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).