Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wakazi wa Kijijizi
cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alipofika
kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(kushoto) akimtwika ndoo ya maji
mmoja wa akina Mama wa Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani, katoka katika kisima cha maji kinachotumia
umeme wa REA baada ya Naibu Waziri kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( pili kushoto) akikata utepe
kuashiria kuwasha umeme katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo,
wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alipofika kuwasha umeme katika kijiji
hicho.
Moja ya kisima cha maji kilichounganishwa na umeme wa mradi wa REA
katika Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo, wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwasha umeme katika kijiji
hicho.*********************
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( pili kushoto) akitoa zawadi ya
mifuko ya saruji kwa viongozi wa serikali za mitaa kusaidia ujenzi wa shule
ya msingi katika kijiji hicho na sehemu ya kusherehekea miaka 58 ya
Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri.
***************************************
Na Zuena Msuya ,Pwani
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amelitaka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) kuhakikisha
hawaruki kijiji katika REA Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaoanza
mapema mwezi Januari 2020 kwa kuwa awamu hii ni ya mwisho
kuunganisha Vijiji.
Mgalu alisema hayo, Desemba 8, 2019 wakati akiwasha umeme katika
Kijiji cha Migude, Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mgalu alifafanua kuwa katika utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu
mzunguko wa Pili ni wa mwisho katika kusambaza umeme vijijini, miradi
itakayofuata ni kusambaza umeme katika Vitongoji, hivyo REA na
TANESCO wahakikishe wanashirikisha Serikali za Mitaa ili kuorodhesha
vijiji vyote kwa umakini na usahihi ili viweze kupatiwa umeme ifikapo
Mwezi, June 2021.
Alieleza kuwa huenda Tanzania inaongoza kwa kuwa ya nchi ya kwanza
kwa nchi za Afrika Mashariki katika kusambaza umeme vijijini, ambapo
mpaka sasa ina vijiji 8115, vilivyounganishwa na umeme kati ya vijiji
12,000, vijiji 4000 vilivyosalia kazi ya kusambaza umeme na
kuwaungaishia wateja inaendelea ili kufikia Mwezi Juni 2020 vijiji 10336
viwe vimeunganishiwa umeme na kubakiwa na vijiji 1,200 ambavyo hivi
vitaendelea kuunganishiwa umeme hadi kufia mwezi June 2021, vijiji
vyote nchini vitakuwa vimeunganishwa na umeme.
“TANESCO na REA, hakikisheni hamuachi kijiji, hii ni awamu ya mwisho
kwa mradi wa REA mzunguko wa tatu, “Hii ndiyo Baba lao”, hatutarudi
nyuma tena kuunganisha vijijini, miradi itakayokuja sasa itakuwa ni maalum
kwa ajili ya vitongoji, hivyo basi mshirikishe serikali za mitaa kuhakikisha
hakuna kinachoachwa nyuma na bei ya kuunganishiwa umeme ni shilingi
27,000, na ni marufuku kuwauzia wateja Nguzo wala LUKU” alisisitiza
Mgalu.
Aidha aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi ya REA, kwa kukubali na kuridhia
maombi ya nyongeza ya Kaya 5000, ambazo zilizomba kuunganishiwa
umeme na zoezi hilo likafanyika kwa Mkoa wa pwani,hivyo alitaka utaratibu
huo uendelee kwa maeneo mengine nchini kwa kuwa miradi hiyo imetumia
gharama kubwa katika kuitekeleza na lengo ni kuwafikia wananchi wote.
Sambasamba na hilo aliitaka TANESCO kuangalia namna bora nzuri ya
kuwawezesha wateja kulipia gharama za kuunganisha umeme katika
majumba yao, ikiwezekana kuwakopesha na baadaye walipie kupitia LUKU
au Ankara zao au kuwawekea utaratibu wa kulipia kidogo kidogo ili kila
mmoja aweze kuunganishwa na umeme.
Aliwaeleza kuwa TANESCO wasikatae fedha pale mteja anapotaka kulipa
kwa awamu, isipokuwa waweke utaratibu mzuri wa walipo hayo kwa lengo
la kumsadia mteja yule ambaye hawezi kuzilipa zote kwa mara moja ili
aunganishiwe umeme.
Alirudia kusema utaratibu wa bei ya shilingi elfu 27,000 uliotolewa na Rais
kwa miradi ya TANESCO inalenga wateja walio vijijini ambapo kuna miradi
ya REA,lakini agizo hilo haliwahusu wateja waliopo kwenye Manispaa na
Majiji katika miradi ya TANESCO inayoendela kutekelezwa kwa sababu
TANESCO inatakiwa ijiendesha kutokana na mapato yake.
Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa serikali inapokea maoni yanayotaka
gharama ya shilingi 27,000 iwe nchi nzima, maoni hayo yatafanyiwa utafiti
kwa kina na kuona namna bora ya kupunguza bei ya kuwaunganishia
umeme wateja waliopo katika Manispaa na Miji ili kila mmoja aweze
kupata huduma hiyo kwa gharama anayoweza kuimudu.
Katika hatua nyingine, Mgalu alitumia fursa hiyo kugawa mifuko 50 ya
saruji isaidie ujenzi wa shule za msingi katika kijiji hicho ikiwa
kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 57 ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Mifuko hiyo ya saruji aliikabidhi kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Ki
jiji cha Migude Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na
baadaye kutembelea shule zenye uhitaji mkubwa vifaa na miundombinu.