Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe, Mhandisi Stella Manyanya amewapongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA kwa kufanya usajili wa Jina la Biashara kwa dakika tano. Ameyasema hayo alipotembelea Banda la BRELA kwenye maonyesho ya Bidhaa za Viwanda yanayoendelea katika Uwanja wa Mwl. J.K Nyerere
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe, Mhandisi Stella Manyanya (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mteja wa BRELA Cheti cha Usajili wa jina la Biashara yake alilosajili na kukamilika ndani ya dakika 5 kwenye Maonesho ya bidhaa za Viwanda (Sabasaba).
Wafanyakazi wa BRELA wakiwa kwenye banda la Maonyesho ya Bidhaa za Viwanda katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere ( Sabasaba) kutoka kushoto ni Hilary Mwenda Afisa Tehama,Yusuph Nakapala Afisa Leseni, Robertha Makinda Afisa Habari na Mawasiliano, Hellen Mhina Msaidizi wa Usajili Mkuu na Ruth Mmbaga Afisa Mwandamizi Msaidizi wa Usajili.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Loy Mhando akimuelezea Naibu Waziri wa Viwanda Na Biashara Mhe, Mhandisi Stella Manyanya majukumu mbalimbali ambayo Wakala inayafanya yakiwemo Usajili wa Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma Hataza pamoja na Leseni za Viwanda.
Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wanawakaribisha katika maonesho ya nne (4) ya bidhaa za Viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salama ambayo yatahitimishwa tarehe 9 Desemba, 2019.