Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, akimtunuku Deus Charles Buma Digrii ya Udaktari wa Falsafa Doctor Of Philosophy (PhD) katika Mahafali ya Kumi na Tatu ya chuo hicho yaliyofanyika jana Muhimbili jijini Dar es salaam Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akiongozana na Maprofesa na Wahadhiri wa Chuo hicho katika maandamano kuelekea katika Mahafali ya Kumi na Tatu ya Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi MUHAS jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wakila kiapo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, akiwa meza kuu pamoja na viongozi na wahadhiri mbalimbali wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katika mahafali ya Kumi na Tatu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi MUHAS Muhimbili jijini Dar es salaam jana