Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mloganzila, Bw.Geofrey Maghembe akizungumza baada ya kupokea msaada wa vitabu vya kiada na kampuni ya kusafirisha mizigo kwa njia ya Anga, Maji na nchi kavu Dow Elef International hivi karibuni.
mwakilishi wa Kampuni ya Dow Elef Bw.Isaac Mdimi akizungumza baada ya kufikisha msaada wa vitabu vya kusomea katika shule ya msingi Mloganzila hivi karibuni.
**********************************
Kampuni ya kusafirisha mizigo kwa njia ya Anga, Maji na nchi kavu Dow Elef International imetoa mchango wa vitabu vya kusomea katika shule ya msingi Mloganzira iliyopo Wilayani Kisarawe kwaajili ya kuunga mkono kampeni ya Tokomeza Ziro.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mloganzila, Bw.Geofrey Maghembe ameishukuru kampuni hiyo kwa mchango walioutoa hivyo anaamini wanafunzi wa shule hiyo watanufaika kwa kiasi kikubwa.
“Katika mkakati wetu wa kuinua taaluma ninaamini kwamba vitabu hivi viasaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza malengo yetu, sisi malengo yetu ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa wa kwanza na kuinua wastani wa shule”. Amesema Bw.Maghembe.
Nae mwakilishi wa Kampuni ya Dow Elef Bw.Isaac Mdimi amesema kuwa wanapenda kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii, hivyo wameona katika Wilaya ya Kisarawe kuna baadhi ya shule zimeendelea kufanya vizuri hivyo wakaamua kuanza kusaidia kutoa vitabu katika shule moja ya msingi Mloganzila ambapo wametoa vitabu vya kiada kwa darasa la tatu na darasa la tano ili kuwawezesha kufanya vizuri katika ufaulu wao.
“Hii ni mojawapo ya Sera ya kampuni kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii basi tumeona na sisi tuungane na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Joketi Mwigolo kumpa ushirikiano kwa hilo ili waendelee kufanya vizuri zaidi”.Amesema Bw.Mdimi.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule hiyo wameshukuru uongozi wa Kampuni ya Dow Elef International kwa msaada walioutoa hivyo wametaka mashirika mengine yajitokeze kwaajili ya kutoa msaada kwani bado miundombinu ya shule yao hayko vizuri.
“Mmetuletea vitabu hivi kwaajili ya kutuongezea maalifa tunawahakikishia kupitia vitabu hivi tutafanya vizuri kama wenzetu waliopita hivyo tunaomba mashirika mengine yaweze kujitokeza kwaajili ya kutoa msaada kwa vifaa vya kufundishia na kuboresha miundombinu ya shule kwani hatuna vyoo na madarasa mazuri”. Amesema Asha Jaffary.