Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa habari huko Ofisini kwake Tunguu kuhusu zoezi la uchangiaji wa Damu Salama litalofanyika Bungi Miembe mingi Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud akizungumza kuhusu zoezi la uchangiaji wa Damu Salama litalofanyika Bungi Miembe mingi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana akimkabidhi Mifuko ya Saruji 10 kwa niabaya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud Mwenyekiti wa Maskani ya Ayoub Muhamed Mahmoud ya Uzi Ng’abwa Talib Khamiss Issa huko Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo Tunguu.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
…………………….
Na Mwashungi Tahir – Maelezo.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amesema mkoa huo unatarajia kukusanya zaidi ya chupa elfu moja na tatu za damu salama katika zoezi la uchangiaji damu linalotarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi huu bungi miembe mingi.
Akizungumza na Waandishi wa habari huko Ofisini kwake Tunguu wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi hilo ambalo litaanza na matembezi kuanzia Kibele hadi Bungi Miembe mingi alisema hatua hiyo imefauatia kuwepo kwa upungufu mkubwa wa damu salama katika kitengo cha damu salama hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watu walio wengi hasa akina mama na watoto.
Amesema maisha ya mwanadamu yanategemea damu hivyo ni vyema kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa lengo la kupata radhi za allah kutokana na kuokoa maisha ya watu.
Aidha amewaomba viongozi mbali mbali wakiwemowa kidini, siasa na wengine kwa ujumla kwani hilo linawahusu watu wote na siola watu maalum.
“Lengo la kutoa Damu salama halilengi kwa watu maalumu litafanyika kwa Makundi yote yakiwemo,Vyama vya siasa, Dini, na Makabila na sio suala la siasa”alisema Ayoub.
Vile vile alisema Wanawake 50 wataojitokeza kutoa damu mwanzo atawazawadia zawadi mbali mbali ikiwepo Chupa za chai na Kanga na Vijana atawazawadia Fulana na Mwamvuli.
Hata hivyo alisema dhamira ya Bonaza hilo ni kuhakikisha damu salama inapatikanwa kwa wingi katika Mkoa huo ili kuondosha changamoto zinazoweza kujitokeza hasa kwa kina mama.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana alikabidhi Mifuko ya Saruji 10 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud kwa ajili ya ujenzi wa Maskani ya Ayoub iliopo Uzi Ng’abwa iliopo Mkoa wa Kusini Unguja.