Home Mchanganyiko KWA MIAKA 15 SASA TANZANIA INAJITOSHELEZA CHAKULA KWA WANANCHI WAKE BILA KUHITAJI...

KWA MIAKA 15 SASA TANZANIA INAJITOSHELEZA CHAKULA KWA WANANCHI WAKE BILA KUHITAJI MSAADA KWA NCHI ZA JILANI-PROF.NYANGE

0

Mratibu wa Mradi wa ASPIRES Prof.David Nyange akitoa Semina kwa wanahabari wa kilimo walioweza kuhudhulia semina semina hiyo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani hivi karibuni.

Wanahabari wa Kilimo wakimsikiliza muwasilishaji wa mada katika semina ya Wanahabari wa Kilimo iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani hivi karibuni.

Bi.Veneranda Baraza Mkulima wa Pilipili Hoho Wilayani Chalinze kata ya Kiwangwa akiwa ndani ya Shamba lake na kuwaonesha wanahabari wa kilimo namna ukulima wa hoho unavyoandaliwa mpaka unapovuna.

Moja ya nanasi likiwa shambani kabla ya mavuna katika moja ya shamba lililopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa PWani.

***************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Inakadiriwa takribani miaka 15 Tanzania imekuwa ikijitosheleza kwa chakula pasipokuhitaji msaada katika nchi za jirani na kuweza kufanya suala la  utapiamlo kushuka kwa miaka 14 hapa nchini. 

Ameyasema hayo leo Mratibu wa Mradi wa ASPIRES Prof.David Nyange katika Semina ya Wanahabari iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani iliandaliwa na Taasisi ya Aspire kwa kushirikiana na USAIDS ili kuweza kuwajengea wanahabari uelewa kuhusu tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo kuhusu Kilimo hapa nchini.

Akizungumza na Wanahabari katika Semina hiyo Prof.Nyange amesema kuwa licha ya changamoto nyingi kuikabili sekta ya Kilimo bado sekta hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa mafanikio makubwa.

“Ukuaji wa Sekta hii bado haijaendana na rasirimali zetu pamoja na fursa zilizopo kwahiyo kadri siku zinavyosonga ndivyo sekta hii imekuwa ikikua kwa kiasi kikubwa”. Amesema Prof.Nyange.

Aidha,Prof,Nyange amesema kuwa wao wamekuwa wakijitahidi kutoa mchango mkubwa katika suala la ushirikiano na majukwaa mbalimbali ya tafiti yaliyopo nchini kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa kwa kiasi kikubwa.

Wakizungumza wakulima wa mbogamboga na wafugaji kwa nyakati tofautitofauti wamesema kuwa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili ni pamoja na upatikanaji wa soko la mauzo.

Bi.Veneranda Baraza Mkulima wa Pilipili Hoho Wilayani Chalinze kata ya Kiwangwa amewataka wote ambao wanahitaji kuingia katika kilimo cha mbogamboga wafahamu kwanza soko linakwendaje,kwani kunaweza kukuletea hasara kubwa kama tu haujaandaa soko la kuuzia mbogamboga zako.

“Unapopanda mazao ya mbogamboga lazima ufahamu kwamba itakapoiva baada ya miezi mitatu kuna soko,kwani unaweza ukapanda mbogamboga ikaiva vizuri sana lakini ukakosa soko ikawa kazi na bure”. Amesema Bi. Veneranda. 

Kwa upande wa wakulima wa Mananasi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamesema kuwa soko la uuza wa mananasi umekuwa mgumu kutokana kuwepo kwa viwanda vichache nchini na uhitaji wake wa nanasi ni mdogo hivyo wakati mwingine inawabidi kuuza kwa bei ndogo ambayo hailingani na mahitaji yao.

Hata hivyo Mmoja wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika Wilaya ya Bagamoyo amesema kuwa kwa upande wake changamoto kubwa ni baadhi ya chanjo kwaajili ya ng’ombe pamoja na malisho.