Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro leo tarehe 05.12.2019 wamepata mafunzo maalum yaliyoendeshwa na maafisa BOT mafunzo hayo yalikuwa yanahusiana na utambuzi wa noti bandia ambapo mafunzo hayo yalihudhuliwa na askari wa vyeo mbalimbali.
Mafunzo hayo yatawajengea askari uwezo wa kutambua noti bandia pia wataweza kutoa elimu kwa wananchi na wao kutambua noti bandia na madhara yake.
Katika mafunzo hayo askari wamejifunza alama mbalimbali zilizomo kwenye noti ambapo kati ya alama hizo zipo alama zinazoweza kuonekana kwa macho na nyingine ambazo huwezi kuziona kwa macho mpaka kifaa maalum pamoja na hayo askari wamepata elimu ya kutofautisha kati ya noti bandia na noti halali.
Mafunzo kazini kwa askari yalifunguliwa na kufungwa na SACP DAVID MISIME wakati anahitimisha mafunzo hayo aliwaasa askari kwamba mafunzo waliyoyapata wakatoe elimu kwa wenzao ambao leo hawakuwepo kutokana sababu za mbalimbali ikiwa ni pamoja na majukumu ya kazi. Pia amewasihi kwenda kutoa Elimu kwa wananchi waweze kupata elimu hiyo muhimu.
Askari walifurahi kupata elimu hiyo na baadhi yao wanadai kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao na hatua za haraka ziweze kuchuliwa ili kudhibiti