Home Mchanganyiko VIONGOZI WATOA TAMKO RUKWA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO

VIONGOZI WATOA TAMKO RUKWA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO

0

Na Mwandishi wetu Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesema kutokana na Mkoa wake kuwa na changamoto ya ukatili dhidi ya watoto amewataka watendaji serikalini wakiwemo wasimamizi wa sheria  kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutenda haki bila kutumia rushwa lakini pia akawataka kuhakikisha kesi zinazohusiana na masuala ya watoto zinakamilika mapema.

Kiongozi huyo wa Mkoa wa Rukwa pia amewataka walimu kote mkoani Rukwa kuhakikisha wanatimiza jukumu la kuwa walezi watoto na kuacha tabia ya kuwa wao ni sehemu ya wachangiaji ukatili kwa watoto kwani baadhi yao wamekuwa wakiwapa mimba wanafunzi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake alipokutana na uongozi wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii ofisini kwake leo kwa lengo la kushirikiana na Mkoa huo katika juhudi za serikali kutokomeza mimba za utotoni hapa Nchini.

Aidha Bw. Wangabo amesema mkoa wake unaungana na nchi nyingine Duniani ili kuhakikisha haki zote za msingi kwa watoto zinatekelezwa ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto lakini akawataka wazazi na walezi kutekeleza wajibu wao ipasavyo ili watoto waweze kuepukana vitendo hivyo.

Askofu Mkuu Jimbo Katoliki Rukwa Askofu Beatus Christian Urasa naye akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto amesema Kanisa Katoliki linaamini mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na kwa vyovyote vile mtoto hapaswi kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Adha Askofu Urasa amesema ili kutokomeza vitendo vya ukatili anawaarika watu wote wenye mapenzi mema kushirikiana ili warudishe maadili mema mahala pake katika jamii na katika familia uku akiwataka wanandoa  kuheshimu utakatifu wa ndoa zao na kuwajibika kwa pamoja kuwalea watoto wao.

Aidha amewataka watoto wote wanaofanyiwa na vitendo vya ukatili kutoa taarifa mara moja katika vyombo vya dora au sehemu inayohusika ili waweza kupata msaada mara moja lakini pia akaongeza kuwa Dawati la Jinsia la Jeshi la polisi linawajibika kutenda haki kwa waanga wa ukatili kwa kushirikiana na watendaji wengine serikalini. 

Katibu wa Muungano wa Makanisa ya Kikristo Mkoani Rukwa Mchungaji John Malaki amewataka watoto wote Nchini kumtegemea Mungu na kutegemea Sala na maombi wawapo nyumbani lakini pia wajiepushe na zawadi na msaada binafsi yenye lengo baya ndani yake ili waweze kuepukana na vitendo vya ukatili .

Mchungaji Malaki pia amewataka wazazi na walezi wajielekeze katika kutimiza mahitaji ya msingi kwa watoto lakini pia watoe malezi mema ili watoto wapate maarifa ya kuwaepusha na vishawishi na ngono lakini pia wasije kuangamia kwa kukosa maarifa kama ilivyo katika maandiko matakatifu ya Biblia.

Aidha Mchungaji Malaki maweataka wanandoa kuacha makubaliano ya kuvunja sheria ambayo upelekea wanandoa kutengana na kusababisha familia kusambalitika akiongeza kuwa wao kama kanisa wanasema wazi kuwa hasara ni kwako mwenyewe unayeamua kuvunja ndoa kisheria.

Aidha Bw. Malaki ameitaka Serikali kusimamia sheria bila huruma ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili hapa Nchini akiamaini kuwa usimamizi wa sheria kwa wanaobainika kutenda vitendo vya kikatli ndio njia pekee ya kutokomeza ukatili dhidi ya watoto Nchini. 

Wakati huo huo Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali ametoa wito kwa wanchi wa Rukwa kuhakikisha mtoto wa kike anapatiwa elimu ya kutosha kwa kumpa fursa ya kujiendeleza kielimu katika mambo ya dunia ilia pate ufahamu wa mazingira yake lakini pia mafunzo ya dini ili aweze kufikia ndoto zake.

Kiongozi huyo wa Dini Mkoani Rukwa amewataka wanaume wote wanaokatiza ndoto za watoto wakike kuwa watajibu mbele ya mwenyezi Mungu kwani Dini ya Kiislam inapinga na inakatiza vitendo viovu vya kuwapa mimba watoto wadogo kwani jambo hilo upelekea watoto hawa kuaribikiwa kimaisha na kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha Shekhe Akilimali amesikitishwa na uwepo wa takwimu zinazoonesha kuwa Rukwa ni miongoni mwa Mkoa mitano yenye kiwango cha juu cha ukatili Nchini na kuhaidi kushirikiana na viongozi wengine wadini Mkoani humo kutumia fursa walizonazo kama viongozi wa juu wa dini kushawishi jamii kuachana na mila potofu zinazopelekea uwepo wa mimba na ndoa za utotoni.  

Pamoja na viongozi wa dini kukemea vitendo vya uakatili Mkoani humo Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia watoto Nchini Bw. Seabastian Kitiku amesema kuwa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii inakusudia kufungua Dawati la Jinsia Mashuleni na kuongeza kuwa Dawati hilo litaundwa na wanafunzi wenyewe kama hatua muhimu itakayowezesha watoto hao kuibua vitendo vya ukatili nje na ndani ya maenep ya shule.