Meneja Mawasiliano wa TBL, Abigail Mutaboyerwa, akiongea juu ya ukatili wa Kijinisia kwa wakazi wa kijiji cha Maneromango tarafara ya Maneromango Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani wakati wa semina iliyoandaliwa na TBL kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Dawati la jinisia Wilaya ya Kisarawe na waadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Duniani.
Wakazi wa Kijiji cha Maneromango Wilaya ya Kisarawe, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa jeshi la Polisi Wilaya ya Kisarawe (OCD) Eva Stesheni wakati alipokuwa akitoa mada ya Ukatili wa Kijinisia kwa wanakijiji hao wakati wa maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.
Wanafunzi wa Sekondari ya Maneronango High School , iliyopo Maneronago Kisarawe wakimsikilza kwa makini Mkuu wa jeshi la Polisi Kisarawe OCD, Eva Stesheni wakati akiwaelimisha njisi ya kujikinga na mimba za utotoni wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Wadau mbalimbali wa masuala ya kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia wakiwa katika picha ya pamoja na wazee mashuhuri wa kijiji cha Meneromango kilichopo Wilaya ya Kisarawe wakati wa maadhimisho ya siku 16 y ak kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.