Mwanafunzi wa Darasa la tano shule ya Msingi ya Chadulu,Nuru Kwangaya,akiimba nyimbo mbalimbali kabla ya kuibuka mshindi wa shindano la uimbaji kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali zilizopo jijini Dodoma walioshiriki kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 lililofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali wakionesha umahiri wao katika tamasha la Mavunde Talent Search 2019 lililofanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa Shindano la Mavunde Talent Search 2019 Bw.Samwel Marwa,akitoa tathimin kwa wanafunzi walioshiriki Tamasha hilo la kuibua vipaji kwa shule za msingi mbalimbali zilizopo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wazazi wakifatilia shindano la wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali zilizopo jijini Dodoma tamasha la Mavunde Talent Search 2019 lililofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobasi Katambi,akizungumza kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dodoma.
Mratibu wa Shindano la Mavunde Talent Search 2019 Bw.Samwel Marwa,akizungumza kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dodoma.
Afisa kutoka Ofisi ya Utamaduni Halmashauri ya jiji la Dodoma Bw.Desdery Kuzenza,akizungumza kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dodoma.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri Jiji la Dodoma Bw.Martin Nkwabi,akizungumza kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dodoma.
Hawa ndo wanafunzi 20 walioshinda shindano kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 ambao wamepata ufadhili wa kusomeshwa bure katika shule ya Ellen White English Medium kutoka kwa Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde
…………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mwanafunzi wa Darasa la tano Nuru Kwangaya,anayesoma shule ya Msingi ya Chadulu ameibuka mshindi wa shindano la uimbaji kwenye tamasha la Mavunde Talent Search 2019 lililofanyika jijini Dodoma.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde,ndiye aliyefadhili shindano hilo ambalo limechukua zaidi ya wanafunzi 500 kutoka shule mbalimbali za msingi zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji katika sekta mbalimbali za Michezo.
Mshindi huyo alitangazwa na Mratibu wa shindano Bw. Samwel Marwa amesema kuwa Nuru ni miongoni mwa wanafunzi 20 walioshinda katika shindano hilo ambao wamepata ufadhili wa kusomeshwa bure katika shule ya Ellen White English Medium.
“Tuna kila sababu ya kumshukuru Mbunge wetu ametoa shilingi milioni 36 kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi hawa,ikiwemo usafiri,chakula,vifaa vya kusomea na Ipad,”alisema Marwa.
Aidha amesema vigezo vilivyotumika kuwachuwa hawa wanafunzi 20 ni muonekano,uwezo wa kujieleza ,mavazi,usafi,umakini wa kusikiliza,kujiamini,kuhimili mchezo na kufundishika.
Akiongea katika shindano hilo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobasi Katambi alitoa agizo kwa idara ya elimu kuhakikisha uhamisho unafanyika mapema ili Januari watoto hao wahamie katika shule hiyo.
“Tumsifu na kumshukuru mbunge wetu kwa moyo huu aliouonyesha,na nilivyozungumza nae amesema wanafunzi hawa 20 waliofadhiliwa leo,wakifanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba bado ufadhili utaendelea kwao,huu ni moyo wa kipekee sana,”amesema Katambi.
Hata hivyo Mhe.Katambia ametoa wito kwa wazazi kutowakatisha tama watoto wao pindi wanapoonyesha vipaji bali wawasaidie kuviendeleza.
Na pia katika ufadhili wa watoto 20 kuwalikuwa na zawadi kwa shule iliyokuwa ya kwanza katika shindano hilo ilipata shilingi laki 500,000,shule ya pili shilingi laki 300,000 na shule ya tatu ni shilingi elfu 20,000.