Home Mchanganyiko JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA...

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA MAUAJI

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu [03] kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la JOHN LUBISI MWAKARUNDWA [62] mkazi wa Kitumba.

Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 03.12.2019 majira ya saa 17:15 jioni huko Kitongoji cha Kitumba, Kijiji na Kata ya Nkunga, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, watu hao walimuua JOHN LUBISI MWAKARUNDWA kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu za kisogoni, taya la kushoto na tumboni.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Makandana – Tukuyu.