Washiriki wa warsha ya siku tatu ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika karakana ya ufundi wa viyoyozi na majokofu katika Chuo cha ufundi – VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu mwelekezi wa mpango wa kupunguza Matumizi ya kemikali jamii ya hydrochlofluocar-cons(HCFCs) kemikali zinazotumika kweny viyoyozi na majokofu, Bwana Marvin Kamurthuzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP) akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya vitendo katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu waRais iliyofanyika VETA-Chang’ombe.
Sehemu ya Washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira wakiwa katika makundi kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika karakana ya ufundi wa viyoyozi na majokofu VETA-Chang’ombe
Washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira wakiwa katika mafunzo ya vitendo juu ya ufungaji wa kiyoyozi kwa njia salama za kimazingira katika karakana ya VETA-Changombe wakati wa mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.